Rais Xi Jinping ahudhuria hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na mwana mfalme wa Saudi Arabia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2022
Rais Xi Jinping ahudhuria hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na mwana mfalme wa Saudi Arabia
Rais wa China Xi Jinping, ambaye yuko ziarani nchini Saudi Arabia, akihudhuria hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Mwanamfalme na Waziri Mkuu wa Saudia Mohammed bin Salman Al Saud kwa niaba ya Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud katika kasri la kifalme huko Riyadh, Saudi Arabia, Desemba 8, 2022. (Xinhua/Xie Huanchi)

RIYADH - Rais wa China Xi Jinping ambaye yuko ziarani nchini Saudi Arabia siku ya Alhamisi alihudhuria hafla ya kumkaribisha iliyoandaliwa Mwanamfalme na Waziri Mkuu wa Saudia Mohammed bin Salman Al Saud kwa niaba ya Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud kwenye kasri la kifalme katika mji mkuu Riyadh.

Gari la Rais Xi, likisindikizwa na walinzi waliokuwa wakiendesha pikipiki na farasi, lilifika katika Ikulu ya Al Yamamah ambapo mwanamfalme wa Saudi alimsalimia Rais wa China kwa furaha.

Viongozi wa nchi hizo mbili waliingia kwenye banda maalumu na bendi ya kijeshi ya kasri la kifalme ikapiga nyimbo za taifa za China na Saudi Arabia.

Akiambatana na mwanamfalme Mohamed bin Salman, Rais Xi alikagua walinzi wa gwaride la heshima, ambao walimkaribisha kwa dhati zaidi Rais wa China kwa jadi za kitamaduni za kushika upanga.

Viongozi Ding Xuexiang, Wang Yi na He Lifeng, miongoni mwa wengine, walihudhuria hafla hiyo

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha