Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2022
Xi Jinping afanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi
Rais wa China Xi Jinping akisalimiana na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi mjini Riyadh, Saudi Arabia, Desemba 8, 2022. (Xinhua/Yao Dawei)

RIYADH - Rais wa China Xi Jinping siku ya Alhamisi alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi mjini Riyadh, Saudi Arabia.

Rais Xi ameeleza kuwa kadiri mazingira ya kikanda na kimataifa yanavyoendelea kupitia mabadiliko na changamano kubwa, umuhimu wa kimkakati na mkubwa wa uhusiano kati ya China na Misri unazidi kudhihirika. Maono na maslahi ambayo China na Misri zinashiriki yanamaanisha kuwa pande hizo mbili zinahitaji kufanya kazi pamoja katika kujenga jumuiya ya China na Misri yenye yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya na kuendeleza zaidi ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Misri.

Rais Xi amesisitiza kuwa China inaunga mkono kithabiti Misri katika kuchagua njia ya maendeleo inayoendana na hali ya kitaifa na katika kulinda mamlaka, usalama na maslahi ya maendeleo ya taifa. Amesema, China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na Misri, kuhakikisha kukamilika kwa muda uliopangwa na ubora wa juu mradi wa treni katika Mji wa “Tarehe 10 Mwezi Ramadhani” na Wilaya ya Kati ya Biashara (CBD) katika mji mkuu mpya wa utawala wa Misri, na kufanya Eneo la Ushirikiano wa Kiuchumi na Biashara la Suez la China na Misri na miradi mingine muhimu ya ushirikiano kufanikiwa.

China iko tayari kuagiza bidhaa bora zaidi kutoka Misri na kupanua ushirikiano katika uwekezaji na mitaji, uzalishaji wa pamoja wa chanjo na anga. Amesema pande hizo mbili zinahitaji kuhimiza Karakana za Luban na kujifunza lugha ya Kichina ili watu wengi zaidi wawe madaraja ya kirafiki kati ya China na Misri, amesema Rais Xi.

Pamoja na kuipongeza Misri kwa kuandaa kwa mafanikio Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Sharm El-Sheikh (COP27), Rais Xi amesema China iko tayari kuongeza ushirikiano na Misri katika Umoja wa Mataifa na kwenye majukwaa mengine ya pande nyingi, na kutetea kwa pamoja ushirikiano wa kweli wa pande nyingi, kushikilia kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa, kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea, na kuhimiza amani na utulivu katika kanda.

Kwa upande wake Rais Sisi amesema kuwa chini ya uongozi madhubuti wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), China imepata mafanikio makubwa ya kimaendeleo na kupata hadhi ya kimataifa. Ametoa pongezi za dhati kwa mafanikio ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliomalizika hivi karibuni.

Rais Sisi amesema upande wa Misri unashikilia kithabiti sera ya kuwepo kwa China moja, na unaunga mkono kithabiti msimamo wa China kuhusu Hong Kong, Xinjiang na masuala mengine yanayohusu maslahi ya kimsingi ya China, na unapinga kithabiti nguvu yoyote ya nje kuingilia katika mambo ya ndani ya China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha