Ndege Kubwa ya Abiria C919 ya Kwanza duniani kuundwa na China yakabidhiwa kwa kampuni ya safari za ndege

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2022
Ndege Kubwa ya Abiria C919 ya Kwanza duniani kuundwa na China yakabidhiwa kwa kampuni ya safari za ndege
(Picha ilitolewa na kampuni ya safari za ndege ya China Eastern.)

Tarehe 9, Desemba, 2022, ndege kubwa ya abiria C919 yenye namba za usajili B-919A imeruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Pudong mpaka Uwanja wa Ndege wa Hongqiao huko Shanghai, China. Hii inaashiria ndege kubwa ya abiria C919 ya kwanza duniani imekabidhiwa kwa mtumiaji wake wa kwanza, yaani kampuni ya safari za ndege ya China Eastern (CEAIR).

Ndege C919 iliyokabidhiwa kwa CEAIR kwa sasa imepakwa rangi na kuchorwa alama maalumu. Kwenye sehemu ya mbele ya ndege hiyo, kuna muhuri wa kichina wenye maneno kwa lugha ya Kichina yasomekayo “ya kwanza duniani” ukifuatiwa na maneno kama hayo kwa Lugha ya Kiingereza.

Ikilinganishwa na ndege za Airbus A320 au Boeing B737, C919 ina viti 158 hadi 168, pamoja na uwezo wa kuruka kwa umbali wa kilomita 4,275 hadi 5,555.

Makadhibiano ya ndege hiyo ya C919 ya kwanza yana umuhimu katika maendeleo ya sekta ya uundaji wa ndege kubwa ya China. Yanaonyesha baada ya miaka 30 hivi, soko la ndege za abiria la dunia limekaribisha ndege kubwa nyingine iliyovumbuliwa upya kabisa. Na kwa kupitia juhudi za kizazi hadi kizazi, soko la la usafiri wa anga la China pia kwa mara ya kwanza litakuwa na ndege kubwa iliyovumbuliwa na China yenyewe.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha