Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Kidijitali yafunguliwa Mkoani Zhejiang, Mashariki mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 12, 2022
Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Kidijitali yafunguliwa Mkoani Zhejiang, Mashariki mwa China
Mfanyakazi akiangalia mfano wa Kiwanda kinachotumia teknolojia ya akili bandia ya 5G+ kwenye Maonyesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Biashara ya Kidigitali huko Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang nchini China, Desemba 11, 2022. Maonyesho hayo ya siku 4 yameanza hapa Jumapili. Takriban kampuni 800 zinazoongoza za biashara ya kidijitali kutoka China na nje ya nchi hiyo zitaonyesha bidhaa na teknolojia zao mpya kwenye maonyesho hayo. (Xinhua/Xu Yu)

HANGZHOU - Maonyesho ya Kwanza ya Kimataifa ya Biashara ya Kidigitali yamefunguliwa Jumapili huko Hangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China.

Mashirika ya kimataifa na makampuni ya biashara kutoka zaidi ya nchi na maeneo 50 yamealikwa kushiriki maonyesho hayo ili kujadili mada mbalimbali muhimu kuhusu biashara ya kidijitali duniani na kusukuma kufungua mlango na ushirikiano wa uchumi wa kidijitali kwa njia ya haraka.

"Kama sehemu muhimu ya uchumi wa kidijitali, biashara ya kidijitali inawakilisha mwelekeo mpya katika maendeleo ya biashara ya kimataifa na ni injini mpya ya ukuaji wa biashara ya kimataifa, ikiingiza nguvu mpya katika ufufuaji na ukuaji wa uchumi wa Dunia," Wu Zhengping, mkuu wa idara ya maendeleo ya biashara ya Wizara ya Biashara ya China amesema.

Maonyesho hayo yenye kaulimbiu inayosema "Kuunganisha Biashara ya Kidijitali kwa Dunia," yanafadhiliwa na Serikali ya Mkoa wa Zhejiang na Wizara ya Biashara ya China. Yataendelea hadi Jumatano wiki hii.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha