Daraja la Tseung Kwan O Cross Bay la Hong Kong lafunguliwa kwa matumizi ya umma (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 12, 2022
Daraja la Tseung Kwan O Cross Bay la Hong Kong lafunguliwa kwa matumizi ya umma
Picha hii iliyopigwa Tarehe 8 Desemba 2022 ikionyesha Daraja la Tseung Kwan O Cross Bay huko Hong Kong, Kusini mwa China. (Picha na Yan Jinwen/Xinhua)

HONG KONG - Daraja la Tseung Kwan O Cross Bay la Hong Kong limefunguliwa kwa matumizi ya umma siku ya Jumapili, na kuwa daraja kuu la kwanza lililojengwa na kampuni ya China Bara pekee huko Hong Kong.

Likiwa ni njia muhimu ya kuvuka bahari katika Ghuba ya Junk Kusini Mashariki mwa mipaka mipya ya Hong Kong, Daraja la Tseung Kwan O Cross Bay, mradi mkuu wa Cross Bay Link, limejengwa na kampuni ya barabara na daraja la China, na ujenzi wake umechukua miaka mine kukamilika.

John Lee, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR), alisema Jumamosi kwenye hafla ya kuzindua Handaki la Tseung Kwan O-Lam Tin na Cross Bay Link kwamba serikali ya HKSAR itashikamana na mbinu inayoongozwa na miundombinu kwa kuanzisha ujenzi wa miradi zaidi ya usafiri na kuboresha mitandao iliyopo, na itatoa mwongozo kuhusu hili mwishoni mwa mwaka ujao.

Daraja hilo la kiungo katika eneo la Tseung Kwan O lina urefu wa takriban kilomita 1.8, ambapo kilomita 1 ni njia ya baharini na daraja la chuma ni sehemu muhimu ya njia ya baharini.

 Kampuni ya barabara na daraja la China lilisema daraja hilo ndilo daraja refu zaidi na lenye upinde wa chuma kizito zaidi huko Hong Kong.

Sehemu za daraja la chuma zilitengenezwa awali katika China Bara na daraja la urefu wa mita 200 liliwasilishwa Hong Kong kutoka Nantong, Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China.

Hii ni mara ya kwanza ambapo "njia ya kuelea juu" imetumika kwa ajili ya ujenzi wa daraja nchini China, na timu ya ujenzi wa mradi pia ilizingatia hali ya mawimbi kwa ajili ya usimamishaji wa daraja.

Mradi huo wa daraja ulitumia njia ya kutengenezwa na kuundwa kwake nje ya eneo la mradi, daraja zima likikamilishwa liwasilishe kwenye eneo la mradi na kulifunga, na ni mafanikio kwamba chuma chenye uzito wa juu wa S690 kinatumika kwa matao ya daraja.

Daraja hilo linakuwa ni njia ya kwanza ya baharini huko Hong Kong yenye njia ya magari, njia ya watembea kwa miguu, njia ya baiskeli na eneo la kutazama mandhari kwa wakati mmoja. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha