Ushahidi zaidi ya 20,000 wa Hatia za Kikosi cha 731 cha jeshi la Japan la uvamizi waonyeshwa kwa mara ya kwanza (12)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 13, 2022
Ushahidi zaidi ya 20,000 wa Hatia za Kikosi cha 731 cha jeshi la Japan la uvamizi waonyeshwa kwa mara ya kwanza
Picha iliyopigwa tarehe 10, Desemba ikionesha Jumba liliokarabatiwa la Makumbusho ya ushahidi wa hatia za kikosi cha 731 cha Jeshi la Japan lililoivamia China. (Xinhua/Zhang Tao)

Tarehe 10, Desemba, wakati wa kuwadia kwa siku ya tisa ya kitaifa ya kuwakumbuka watu waliouawa katika Mauaji wa Nanjing, mradi wa kukarabati upya Jumba la Makumbusho ya ushahidi wa hatia za kikosi cha 731 cha Jeshi la Japan lililoivamia China (Kwa ufupisho "kikosi cha 731") umekamilika, ambako mabaki mapya na nyaraka mpya za kihistoria zaidi ya 20,000 vinaoneshwa kwa mara ya kwanza. Wataalam wamesema, ushahidi huo mpya wenye nguvu umeongeza ushahiri mpya usiofutika juu ya hatia za kikosi cha 731 za kufanya majaribio ya miili ya binadamu, kutafiti na kutengeneza silaha ya bakteria, kufanya vita vya bakteria na hatia nyingine kadha wa kadha, na umekamilisha zaidi mnyororo wa ushahidi. (Picha/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha