Messi na Alvarez waipeleka Argentina kwenye Fainali ya Kombe la Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 14, 2022
Messi na Alvarez waipeleka Argentina kwenye Fainali ya Kombe la Dunia
Julian Alvarez (Kulia) wa Argentina akishangilia pamoja na Lionel Messi baada ya kuifungia timu yake bao la pili kwenye mchezo wa Nusu Fainali kati ya Argentina na Croatia wa Kombe la Dunia la FIFA 2022 uliochezwa Uwanja wa michezo wa Lusail mjini Lusail, Qatar, Desemba 13, 2022. (Xinhua/Xu Zijian)

LUSAIL, Qatar - Julian Alvarez alifunga mara mbili na Lionel Messi akafunga penalti kipindi cha kwanza hivyo kuifanya Argentina kutinga fainali ya Kombe la Dunia kwa ushindi mnono wa 3-0 dhidi ya Croatia siku ya Jumanne.

Messi aliifungia Argentina dakika ya 34 ya mchezo kwa shuti la penati iliyotolewa na mwamuzi baada ya kipa wa Croatia Dominik Livakovic kumgonga Alvarez aliyekuwa akielekea kufunga bao.

Alvarez alifanya matokeo kuwa 2-0 alipopokea mpira akiwa kwenye nusu ya uwanja kabla ya kuanza kukimbia peke yake na kufunga kwa karibu.

Mshambulizi huyo wa Manchester City aliongeza bao lake binafsi la pili na la tatu kwa timu yake katika usiku wa jana kwa kufunga bao la karibu baada ya Messi kumchenga na kumpita mlinzi wa Croatia na kuvuka mstari wa kulia.

Ilikuwa ni kuonesha uwezo mwingine wa aina yake wa Messi katika kusakata kabumbu, ambaye anaonekana kama mtu aliye kwenye misheni katika mechi yake ya tano, na ambayo inawezekana ikawa ya mwisho, katika mashindano hayo ya soka.

Mshindi huyo mara saba wa tuzo ya Ballon d'Or sasa ametikisa nyavu mara tano na kutoa pasi tatu za mabao akiwa Qatar 2022 na goli lake hilo la jana limemfanya kumzidi Gabriel Batistuta kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Argentina wa Kombe la Dunia akiwa na mabao 11.

Argentina itacheza na mshindi wa nusu fainali nyingine ya leo Jumatano kati ya mabingwa watetezi Ufaransa na Morocco katika fainali siku ya Jumapili.

Timu zote zilijitahidi kutengeneza hatari mapema na ilichukua dakika ya 25 mchezo kupiga shuti la kwanza lililolenga lango: kazi ndogo kutoka kwa Enzo Fernandez ambayo hata hivyo Livakovic alipoteza.

Wakati Croatia walitawala mpira, sehemu kubwa ilikuwa kwenye nusu yao, na kuwaacha washambulizi wake Ivan Perisic na Andrej Kramaric wakiwa wametengwa zaidi katika mashambulizi.

Argentina walisonga mbele katika dakika ya 32 baada ya Luka Modric kupoteza umiliki wa mpira. Fernandez alimtafuta na kumpasia Alvarez, ambaye alipiga shuti juu ya Livakovic kabla ya beki huyo anayekipiga Dinamo Zagreb kupunguza hatari. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha