Watu wanasherehekea mavuno kwa ala ya muziki ya jadi huko Guizhou, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 14, 2022
Watu wanasherehekea mavuno kwa ala ya muziki ya jadi huko Guizhou, China

Tarehe 12, Desemba, katika Kijiji cha Basha cha kabila la Wamiao, wilaya ya Congjiang ya Mkoa wa Guizhou, China, Wamiao walicheza ngoma ya Lusheng, kufanya mashindano ya kupiga ala ya Lusheng na shughuli nyingine za jadi, ili kusherehekea sikukuu ya jadi ya Lusheng, ambayo ni ala ya muziki ya jadi ya kabila hilo.

Sikukuu ya Lusheng ni sikukuu ya jadi inayosherehekewa kwa shangwe zaidi katika maeneo ya kabila la Wamiao. Watu husherehekea sikukuu hiyo ifikapo tarehe 19, Novemba kila mwaka, ambapo vijana huwasiliana na kueleza mapenzi yao, na watu wakipiga ala ya Lusheng kwa kutakia salama na mavuno.

Kijiji cha Basha cha kabila la Wamiao kinahifadhi mila na desturi za zama za kale na mtindo wa kale wa uzalishaji, kikiwa kijiji kipekee ambacho wanakijiji wake wanaruhusiwa kubeba bunduki, hivyo kimesifiwa kuwa “kabila la mwisho la wanabunduki nchini China”.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha