“ Tamasha la 20 la Theluji na Barafu” laanzishwa Urumqi, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 15, 2022
“ Tamasha la 20 la Theluji na Barafu” laanzishwa Urumqi, China
Picha ikionesha ufunguzi wa Tamasha la 20 la Theluji na Barafu la Njia ya Hariri huko Urumqi, China. (Picha ilipigwa na Li Xinyang/People’s Daily Online)

Tarehe 14, Tamasha la 20 la Theluji na Barafu la Njia ya Hariri lilifanyika Urumqi, Xinjiang, China, likiashiria kuanzishwa rasmi kwa shughuli za utalii za majira ya baridi ya mwaka 2022-2023 za mji huo.

Tamasha hilo linalenga kuwavutia watu kushiriki zaidi katika michezo ya theluji na barafu kwa kupitia kuonyesha mazingira ya theluji na barafu ya Urumqi.

Habari zinasema, wakati wa tamasha hilo, mji wa Urumqi umeandaa shughuli 69 mfululizo, huku baadhi ya uwanja wa michezo ya kuteleza kwenye theluji mjini Urumqi utapunguza bei kwa wakazi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha