Tazama wanakijiji hawa wanavyopenda soka kwa namna gani

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 15, 2022
Tazama wanakijiji hawa wanavyopenda soka kwa namna gani
Tarehe 7, Desemba, timu za mpira wa miguu ya Kijiji cha Longnai na Kijiji cha Yonghe zikicheza michezo katika Wilaya inayojiendesha ya Cangyuan ya kabila la Wawa, Mji wa Lincang, Mkoa wa Yunnan.

Katika Kijiji cha Longnai, Wilaya inayojiendesha ya Cangyuan ya kabila la Wawa, Mji wa Lincang, Mkoa wa Yunnan, kuna wakulima wengi wanaopenda kucheza mpira wa miguu: wanafanya kazi mchana na kucheza mpira wa miguu jioni, mara nyingi hadi saa nne usiku. Watu hao wanafanya shughuli mbalimbali, lakini wote wanapenda mpira wa miguu.

Mwaka 2003, Kijiji cha Longnai kilianzisha timu yake ya mpira wa miguu, Bao Zhikun aliyependa mpira wa miguu tangu alipokuwa mtoto alikuwa mkuu wa kwanza wa timu hiyo. Mwaka 2016, mwanakijiji Bao Aigai alichukua jukumu la mkuu wa timu hiyo. Miaka mitatu baadaye, aliiongoza timu hiyo kutwaa taji la ubingwa.

Mwaka 2020, Kijiji hiki kikitegemea mradi wa wilaya kilijenga kiwanja cha mpira wa miguu cha wanamichezo watano, ambacho nyuma yake ni milima na kinazungukwa na mashamba ya mazao. Ili kuongeza muda wa kucheza, wanakijiji walichangisha fedha wenyewe na kufunga taa nane kwenye kiwanja hicho . Kila ifikapo usiku, hapa panakuwa mahali penye mwanga zaidi ndani ya eneo la maili kumi. Timu za maeneo mengine pia zilikuja kucheza, hasa katika wakati wa wikiendi, kiwanja hicho hujazwa na watu wengi.

Katika miaka ya hivi karibuni, wanafunzi wengi wa kijiji hicho wameendelea na masomo katika vyuo vikuu. Baadhi yao walisoma katika kozi ya michezo, na baada ya kuhitimu masomo walirudi kijijini kuwa makocha wa mpira wa miguu. Wakati timu ya mpira ilipokuwa na mashindano, wanakijiji wengi zaidi walikwenda kiwanjani kuwapigia jeki wachezaji, na pia walilipa wenyewe kwa kutoa huduma mbalimbali kwa wachezaji.

Jambo linalofurahisha Bao Aigai ni kuwa kila mara timu ilipokwenda nje kucheza michezo, miongoni mwa watu waliokuja kuwapigia jeki, watoto kadhaa huonekana. Alisema kuwa watoto hao ni matumaini ya timu ya mpira wa miguu ya Kijiji cha Longnai, iko siku , watoto hao wataweza kukiwakilisha Kijiji cha LongNai kusimama kwenye jukwaa la juu zaidi.

(Mpiga picha: Jiang Wenyao/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha