Picha: Ujenzi wa reli ya mwendo kasi ya Eneo Jipya la Xiong’an-Uwanja wa Ndege wa Daxing wa Beijing (R1) chini ya ardhi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 16, 2022
Picha: Ujenzi wa reli ya mwendo kasi ya Eneo Jipya la Xiong’an-Uwanja wa Ndege wa Daxing wa Beijing (R1) chini ya ardhi
Picha iliyopigwa kutoka angani ikionesha ujenzi wa Reli ya mwendo kasi kati ya Eneo Jipya la Xiong’an na Uwanja wa Ndege wa Daxing wa Beijing. (Picha ilipigwa na Li Zhaomin/People’s Daily Online)

Reli ya mwendo kasi kati ya Eneo Jipya la Xiong’an na Uwanja wa Ndege wa Daxing wa Beijing (R1) inatoka sehemu ya mwanzo wa ujenzi ya Eneo Jipya la Xiong’an, ikipita Mji wa Langfang wa Mkoa wa Hebei, halafu kufika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Daxing wa Beijing, ikiwa na urefu wa jumla wa kilomita 86.26. Baada ya ujenzi wa reli ya R1 kukamilika, watu walioko eneo la Xiong’an wataweza kufika Uwanja wa Ndege wa Daxing wa Beijing kwa kuchukua dakika 30 tu.

Reli ya R1 ni reli kuu katika mtandao wa reli za mwendo kasi wa eneo jipya la Xiong’an uliopangwa. Tarehe 14, Desemba, mwandishi wa Habari alikwenda sehemu ya ujenzi wa reli ya R1 chini ya ardhi, akiona wafanyakazi wakifanya kazi katika hali motomoto, ili kuhakikisha ujenzi wa mradi huo usongee mbele kwa hatua madhubuti.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha