Panda Eimei ateuliwa kuwa Mjumbe Maalumu wa urafiki wa China na Japan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2022
Panda Eimei ateuliwa kuwa Mjumbe Maalumu wa urafiki wa China na Japan
Panda Eimei akiwa katika picha kwenye Adventure World, bustani ya burudani huko Shirahama, Mkoa wa Wakayama nchini Japan, Desemba 17, 2022. Eimei, panda mkubwa ambaye ameishi Japan kwa miaka 28, ameteuliwa kuwa mjumbe maalum wa urafiki wa China na Japan huko Magharibi mwa Japan siku ya Jumamosi. (Xinhua/Jiang Qiaomei)

SHIRAHAMA, Japan – Panda Eimei ambaye ameishi Japani kwa miaka 28, ameteuliwa kuwa mjumbe maalum wa urafiki wa China na Japan huko Magharibi mwa Japan siku ya Jumamosi.

Balozi Mdogo wa China mjini Osaka, Japan Xue Jian ametangaza uteuzi huo katika hafla iliyofanyika Jumamosi huko Adventure World, bustani ya burudani huko Shirahama, Mkoa wa Wakayama nchini Japan, ambapo panda hukaa.

Eimei, au Yong Ming kwa Lugha ya Kichina, ni panda dume mwenye umri wa miaka 30 na ni panda mkubwa zaidi anayeishi Japani. Akiwa alitoka China Mwaka 1994, ni baba wa watoto 16 wa panda waliozaliwa katika eneo la Adventure World, akiweka rekodi ya dunia ya kuwa panda mkubwa zaidi kuwahi kufugwa kwa mafanikio akiwa uhamishoni.

Akieleza kuwa mwaka huu inatimia miaka 50 tangu kurejea kawaida kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Japan na ziara ya kwanza ya panda nchini Japan, Xue amesema kama ishara ya urafiki kati ya China na Japan, panda huyo ana nafasi ya pekee katika kuhimiza urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili na kuendeleza uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

"Natumai watu wengi zaidi wa Japan wanaweza kugeuza upendo kwa panda kuwa upendo wa ubinadamu," Xue amesema, akitumai kuwa watu wengi zaidi wa Japan wanaweza kujisikia karibu na China, nchi ya asili ya panda, kupitia uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizo mbili uliojengwa na panda.

Shukrani kwa ushirikiano wa kirafiki kati ya Adventure World na kituo cha utafiti wa uzalishaji wa panda katika Mkoa wa Sichuan nchini China, Wakayama na Sichuan zilianzisha uhusiano wa kirafiki wa mkoa na mkoa Januari mwaka huu, amesema Shuhei Kishimoto, gavana wa Mkoa wa Wakayama, katika hotuba ya maandishi.

Katika siku zijazo, Mkoa wa Wakayama utaendelea kuhimiza uhusiano wa kirafiki ulioanzishwa na Eimei na kujitahidi kukuza mabadilishano kati ya Japan na China, amesema gavana huyo.

Adventure World imetangaza kwamba Eimei atarejea katika kituo cha utafiti cha Chengdu cha ufugaji wa panda Mwezi Februari mwaka ujao pamoja na watoto wake majike mapacha Ouhin na Touhin. Kutakuwa na panda wanne tu katika bustani hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha