Kijiji cha jadi cha Yulin,Guangxi chaonesha nguvu mpya ya uhai

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 19, 2022
Kijiji cha jadi cha Yulin,Guangxi chaonesha nguvu mpya ya uhai
Picha hii ikionesha Kijiji cha Gaoshan ambacho ni“Kijiji cha jadi cha China”katika Mtaa wa Chengbei, Eneo la Yuzhou la Mji wa Yulin, Mkoa wa Guangxi. (Mpiga picha: Fu Huazhou/Tovuti ya Gazeti ya Umma)

Katika siku za hivi karibuni, watu wengi walikuja Kijiji cha Gaoshan katika Mtaa wa Chengbei, Eneo la Yuzhou la Mji wa Yulin, Mkoa wa Guangxi ili kutembelea kijiji hiki chenye majengo mengi ya Enzi za Ming na Qing yenye historia ndefu.

Katibu wa Tawi la Kamati ya Chama ya Kijiji cha Gaoshan, Mou Ying alisema kuwa Kijiji cha Gaoshan kina historia ya zaidi ya miaka 560 na kina nyumba za makazi ya kale zaidi ya 150, ambayo ni moja ya majengo makubwa ya kale ya Enzi za Ming na Qing huko Guangxi, na kijiji hicho kinafuata mila na desturiza aina mbalimbali.

Katika miaka ya hivi karibuni, Kijiji cha Gaoshan kilifanya juhudi za kuboresha mazingira ya kijiji ili yawe na usafi zaidi , pia kilitegemea nguvu yake bora ya rasilimali na kuhamasisha wanakijiji kutia saini“Makubaliano ya Ulinzi na Uhuishaji wa Nyumba za Makazi ya Kale za Kijiji cha Gaoshan”, kikifanikiwa kuweka mahekalu 13 ya kale ya ukoo na nyumba zaidi ya 150 za makazi ya kale kwenye ushirika wa uchumi wa wanakijiji chini ya uongozi wa Tawi la Kamati ya Chama ya Kijiji cha Gaoshan ili kuzihifadhi na kuzihuisha vizuri.

Kijiji cha Gaoshan kilifanya shughuli mbalimbali za utamaduni zinazopendwa na watu, kama vile usomaji wa vitabu vizuri vya zamani, na matamasha kikionesha hali ya ustawishaji wa vijiji. Pia kilianzisha madarasa ya Sanaa ya ukataji wa karatasi n.k. ili kuenzi mila na desturi za jadi.

Mou Ying alisema kuwa Kijiji cha Gaoshan kina historia ndefu, urithi wa kitamaduni na mila na desturi nzuri za familia, kijiji hicho kitatumia ipasavyo rasilimali hizi bora, kufanya juhudi za kutafuta njia mpya za kukuza utamaduni, kuendeleza kwa nguvu shughuli za utalii vijijini, na kukuza na kuimarisha uchumi wa kijiji, kuwaongoza wanakijiji kuanzisha biashara ili kuongeza mapato yao, na mwishowe kuhimiza kikamilifu ustawishaji wa vijiji.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha