Uvuaji wa samaki katika majira ya baridi Wan’an, Jiangxi (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 27, 2022
Uvuaji wa samaki katika majira ya baridi Wan’an, Jiangxi
Mvuvi akionesha samaki aliyemvua muda huo. (Xinhua)

Siku za hivi karibuni, shughuli za kuvua samaki katika majira ya baridi zinafanyika katika Kijiji cha Changqiao cha Mji Mdogo wa Shaping wa Wilaya ya Wan’an ya Mkoa wa Jiangxi, nchini China, meli zaidi ya 20 za kuvua samaki zikipitapita kwenye mto.

Katika miaka ya hivi karibuni, wilaya ya Wan’an imefuata wazo la “ikolojia+” katika kuendeleza shughuli za utalii, ikihimiza kwa nguvu shughuli za utalii wa majini na sekta nyingine, kupanua minyororo ya sekta ya uvuvi na kuongeza shughuli za utalii zinazowavutia watu.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha