Reli inayounganisha Miji ya Chengdu na Kunming nchini China yaanza kufanya kazi kikamilifu (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 27, 2022
Reli inayounganisha Miji ya Chengdu na Kunming nchini China yaanza kufanya kazi kikamilifu
Picha hii iliyopigwa Tarehe 24 Desemba 2022 ikionyesha treni ya mwendo kasi ya Fuxing ikifanya majaribio kabla ya kufunguliwa kwa Reli mpya ya Chengdu-Kunming katika Eneo la Mianning, Mkoa wa Sichuan nchini China. (Xinhua/Wang Xi)

CHENGDU - Reli ya mwendokasi inayounganisha Chengdu na Kunming, miji miwili mikubwa Kusini Magharibi mwa China, sasa inafanya kazi kikamilifu baada ya kufunguliwa kwa sehemu yake ya mwisho siku ya Jumatatu.

Ikiwa imeundwa kukimbia kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa, njia hiyo mpya yenye urefu wa kilomita 915, ambayo inakaribia kwenda sambamba na reli ya kuunganisha maeneo kati ya Chengdu na Kunming, inatarajiwa kupunguza muda wa kusafiri kutoka saa 19 hadi saa 7.5.

Reli hiyo mpya inapita miji na wilaya mbalimbali, kama vile Chengdu, Meishan, Leshan, Liangshan na Panzhihua katika Mkoa wa Sichuan, na Chuxiong na Kunming katika Mkoa wa Yunnan.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha