Karakana za Luban za China zasaidia kutoa mafunzo kwa wahandisi wa siku zijazo wa Misri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 28, 2022
Karakana za Luban za China zasaidia kutoa mafunzo kwa wahandisi wa siku zijazo wa Misri
Watu wakipokea mafunzo katika eneo la mafunzo ya teknolojia ya matumizi na ukarabati wa magari kwenye Karakana ya Luban katika Chuo Kikuu cha Ain Shams huko Cairo, Misri, Desemba 21, 2022. Kwenye karakana katika Chuo Kikuu cha Ain Shams huko Cairo, baadhi ya wanafunzi wa uhandisi wamekuwa wakifunzwa kuhusu jinsi ya kutumia G-code, lugha ya programu, kuunda kidhibiti cha kiotomatiki cha mashine. Karakana hiyo, inayojulikana pia kwa jina la "Kituo cha Luban cha Misri cha Mafunzo ya Ufundi Stadi," ni mojawapo ya mifano mingi ya ushirikiano wa elimu kati ya China na Misri. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

CAIRO - Kwenye karakana katika Chuo Kikuu cha Ain Shams cha Cairo, baadhi ya wanafunzi wa uhandisi wamekuwa wakifunzwa kuhusu jinsi ya kutumia G-code, lugha ya programu, kuunda kidhibiti cha kiotomatiki cha mashine.

Karakana hiyo, inayojulikana pia kwa jina la "Kituo cha Luban cha Misri cha Mafunzo ya Ufundi Stadi," ni mojawapo ya mifano mingi ya ushirikiano wa elimu kati ya China na Misri.

Ikiwa ilianzishwa na Chuo cha Ufundi cha Tianjin Light Industry cha China, Chuo cha Ufundi wa Usafirishaji cha Tianjin na Chuo Kikuu cha Ain Shams cha Misri mwishoni mwa Mwaka 2020, karakana hiyo kubwa, yenye kuchukua ukubwa wa eneo la karibu mita za mraba 1,200, hutoa mafunzo kwa usakinishaji wa udhibiti wa nambari za kompyuta (CNC), teknolojia za nishati mpya na teknolojia ya matumizi na ukarabati wa magari.

Yomna Osama, mwanafunzi mwandamizi, anasema kwamba amejifunza mengi kutokana na mafunzo aliyopata katika Karakana ya Luban kuhusu muundo wa CNC, sehemu zake, utatuzi na ukarabati.

"Pia tumejifunza G-code, lugha ya programu ambayo mashine inaelewa, na mimi binafsi ninaitumia katika mradi wangu wa kuhitimu," mhandisi huyo ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Profesa Mohamad Ahmed Awad, mkurugenzi wa karakana hiyo, anasema kuwa kituo hicho cha elimu na mafunzo kinawapa wanafunzi nafasi ya kutumia kwa vitendo kile wanachojifunza kinadharia.

"Karakana inawakilisha kiungo muhimu sana kati ya elimu ya kitaaluma na kazi za vitendo za baada ya kuhitimu kwenye viwanda mbalimbali," mkurugenzi huo ameliambia Xinhua.

Eneo la mafunzo ya nishati mpya huwapa wanafunzi mifumo minne na maiga kwa ajili ya uzalishaji wa umeme kwa nishati ya upepo, wakati sehemu ya mafunzo ya ukarabati wa magari ina viigaji halisi na vifaa vya ukarabati wa magari yanayotumia nishati ya mafuta, taratibu na mifumo ya ukarabati.

Karakana ya Luban katika Chuo Kikuu cha Ain Shams siyo pekee nchini Misri. Karakana nyingine ya Luban imefunguliwa hivi karibuni katika Shule ya Juu ya Ufundi wa Ukarabati huko Cairo.

"Ushirikiano kati ya Misri na China unaongezeka katika sekta ya elimu, hasa elimu ya ufundi wa kazi," Mohamed Megahed, Naibu Waziri wa Elimu wa Misri ameliambia Xinhua. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha