China yarusha satelaiti ya majaribio ya anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 30, 2022
China yarusha satelaiti ya majaribio ya anga ya juu
Roketi ya Long March-3B iliyobeba satelaiti ya Shiyan-10 02 ikiruka kutoka kwenye Kituo cha Kurusha Satelaiti cha Xichang Mkoa wa Sichuan, Kusini Magharibi mwa China, Desemba 29, 2022. (Photo by Hu Xujie/Xinhua)

XICHANG - China siku ya Alhamisi imerusha roketi ya Long March-3B, ikiitumia kuweka satelaiti mpya ya majaribio kwenye anga ya juu.

Roketi hiyo iliruka saa 6:43 Mchana (Saa za Beijing) kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Xichang Kusini-Magharibi mwa China na kubeba satelaiti ya Shiyan-10 02 hadi kwenye obiti iliyopangwa mapema.

Shiyan inamaanisha "majaribio" kwa Lugha ya Kichina. Satelaiti mpya ya Shiyan iliyorushwa itatumika kwa ajili ya uthibitishaji wa obiti wa teknolojia mpya za anga ya juu, kama vile ufuatiliaji wa mazingira ya anga.

Hii imekuwa ni kazi ya 458 ya safari ya kwenye anga ya juu kwa kutumia mfululizo wa roketi za Long March.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha