Reli mpya ya mwendo kasi yaanza kufanya kazi Kaskazini Magharibi mwa China (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 30, 2022
Reli mpya ya mwendo kasi yaanza kufanya kazi Kaskazini Magharibi mwa China
Kondakta wa treni wakisubiri treni namba D2763 kuondoka katika Stesheni ya Reli ya Zhongwei Kusini katika Mji wa Zhongwei, Mkoa unaojiendesha wa Ningxia, Kaskazini-Magharibi mwa China, Desemba 29, 2022. (Xinhua/Feng Kaihua)

LANZHOU - Njia mpya ya reli ya mwendo kasi yenye urefu wa kilomita 219, inayounganisha miji ya Zhongwei na Lanzhou Kaskazini-Magharibi mwa China, imeanza kufanya kazi siku ya Alhamisi.

Ikiwa imeundwa kukimbia kwa kasi ya kilomita 250 kwa saa, reli hiyo mpya inayounganisha njia ya reli ya Yinchuan-Zhongwei, imepunguza muda wa kusafiri kati ya Yinchuan na Lanzhou, miji mikuu ya Mkoa unaojiendesha wa Ningxia na Mkoa wa Gansu, hadi chini ya saa tatu.

Reli hii ya mwendo kasi pia inakamilisha sehemu ya mwisho ya njia ya reli inayounganisha mikoa ya Shaanxi, Gansu na Ningxia.

Njia hii ya reli pia inaboresha zaidi mtandao na ufikiaji wa reli ya mwendo kasi kwani inapita kwenye miji mingi mikubwa katika maeneo matatu ya ngazi ya mkoa, amesema Wang Dalin, Afisa wa Shirika la Reli la China, Tawi la Lanzhou.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha