China yapiga hatua kuharakisha uzalishaji wa kilimo nchini Uganda

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2023
China yapiga hatua kuharakisha uzalishaji wa kilimo nchini Uganda
Wafanyakazi wenyeji wakitembea karibu na madimbwi ya samaki katika Kituo cha Utafiti na Maendeleo ya Mazao ya Majini huko Kajjansi, Wilaya ya Wakiso, Uganda, Desemba 21, 2022. (Picha na Hajarah Nalwadda/Xinhua)

WAKISO, Uganda - Siku moja katika Mwezi Disemba yenye joto kali katika Wilaya ya Wakiso katika Mkoa wa Kati nchini Uganda, mtaalam wa kilimo wa China Chen Taihua mwenye umri wa miaka 56, akitazama madimbwi ya samaki katika kituo cha kilimo kilichojengwa na Wachina, alikuwa akifikiria sana jinsi somo kutoka China linaweza kutekelezwa katika maeneo ya vijijini Uganda ili kuwawezesha mamilioni ya watu kuondokana na umaskini.

Huku upepo kutoka Ziwa Viktoria lililo karibu ukipoza hali joto kali ya mchana, Chen hakuweza kujizuia kuzungumzia maliasili ya maji na ardhi ya kilimo ambayo Uganda inayo.

Wakati akiwalisha samaki hao, Chen aliliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi majuzi kwamba katika utajiri wa maliasili ya Uganda, ambao ukitumiwa ipasavyo, unaweza kuboresha maisha ya Waganda.

Chen anapitia njia ambayo wataalam wengine wa China wamechukua katika kusaidia Uganda. Takwimu za Wizara ya Kilimo, Sekta ya Wanyama na Uvuvi ya nchini humo (MAAIF) zimeonesha kuwa, zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wanapata riziki zao kutokana na kilimo.

China, kupitia makubaliano ya pande tatu na Uganda na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), ilituma timu ya wataalam katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kubadilishana uzoefu na wakulima wadogo kuhusu namna bora ya kuboresha uzalishaji wa kilimo kwa kutumia teknolojia zinazofaa. Ushirikiano huo uko chini ya mfumo wa Mpango wa FAO na Ushirikiano wa China wa Kusini-Kusini ambao sasa uko katika awamu ya tatu nchini Uganda.

Awamu ya kwanza na ya pili, kwa mujibu wa MAAIF, iliwezesha uhamishaji wa teknolojia na kuwezesha uboreshaji wa uzalishaji na tija wa sekta ndogo za mazao, mifugo na uvuvi.

Wakati wa awamu hizo, aina ya mpunga chotara wa China na aina ya mtama wa China ulitambulishwa kwa wakulima. Takwimu za MAAIF zimeonesha kuwa, Mpunga huo wa chotara hutoa takriban tani 10 kwa hekta ikilinganishwa jamii za mpunga wa kienyeji zilizoborehwa ambazo hutoa tani 3.5 na 2.5 kwa hekta.

Zhang Xiaoqiang, mkuu wa timu ya kilimo ya China ya awamu ya tatu anasema timu hiyo inalenga kuwasogeza wakulima wenyeji kuangalia kilimo kwa njia ya kibiashara badala ya kujikimu.

"Katika awamu ya tatu, tunataka kukuza uwekezaji katika sekta ya kilimo, bidhaa za ubora wa juu, na kuzileta katika soko la China. Pia tunahimiza makampuni zaidi ya China kuwekeza nchini Uganda, na kuleta mnyororo wao wote wa thamani," Zhang amesema.

Peter Muyimbo, mratibu wa awamu ya tatu kwa upande wa Uganda, amesema awamu hiyo imepangwa ili kufanya uzalishaji wa kilimo kuwa wa kibiashara kwa lengo la kuongeza mauzo ya nje kwenye soko la China.

"Tunaenda kuongeza uzalishaji wa mpunga chotara wa China, mtama, uzalishaji wa mifugo ambapo tunashughulika na uzalishaji wa mbuzi, hasa mbuzi wa masikio makubwa. Pia tutakuwa na uhamisho wa kiinitete hasa katika uzalishaji wa mazao ya maziwa, pia tutakuwa na malisho," amesema Muyimbo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha