Mzigo unaosafirishwa kwa Meli kwenye Bwawa la Magenge Matatu wafikia rekodi mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2023
Mzigo unaosafirishwa kwa Meli kwenye Bwawa la Magenge Matatu wafikia rekodi mpya
Picha hii iliyopigwa Januari 2, 2023 ikionyesha meli zikipitia kwenye eneo maalumu la meli lenye safu tano la Bwawa la Magenge Matatu huko Yichang, Mkoa wa Hubei katikati mwa China. Mzigo unaosafirishwa kwa Meli kwenye Bwawa la Magenge Matatu, mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya maji duniani, ulifikia rekodi mpya Mwaka 2022, Mamlaka ya Usafirishaji ya Magenge Matatu imesema Jumatatu. Jumla ya mizigo yote inayopita kwenye mradi ulifikia tani milioni 159.8 Mwaka 2022, ikiwa ni ongezeko la asilimia 6.12 mwaka hadi mwaka. Mwaka 2022, shehena ya mzigo iliyopita kwenye mradi huo ilikuwa tani milioni 159.65, ongezeko la mwaka hadi mwaka la asilimia 6.53. Wakati huo huo, mzigo uliopita kwenye eneo maalumu la meli lenye safu tano kwenye bwawa hilo ulifikia tani milioni 156.18, ongezeko la asilimia 6.65 mwaka hadi mwaka. (Picha na Wang Gang/Xinhua)

WUHAN - Mzigo unaosafirishwa kwa meli kwenye Bwawa la Magenge Matatu, mradi mkubwa zaidi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya maji duniani, ulifikia rekodi mpya Mwaka 2022, Mamlaka ya Usafirishaji ya Bwawa la Magenge Matatu imesema Jumatatu.

Jumla ya mizigo yote inayopita kwenye mradi huo ilifikia tani milioni 159.8 mwaka 2022, na ilipata ongezeko la asilimia 6.12 mwaka hadi mwaka. Mwaka 2022, shehena ya mizigo iliyopita kwenye bwawa hilo ilikuwa tani milioni 159.65, na kufikia ongezeko la asilimia 6.53. Wakati huo huo, mzigo wa uliopita kwenye eneo maalumu la meli lenye safu tano kwenye bwawa hilo ulifikia tani milioni 156.18, na kufikia ongezeko la asilimia 6.65.

Bwawa la Magenge Matatu ni mfumo wa kudhibiti maji unaofanya kazi nyingi, unaojumuisha bwawa la urefu wa mita 2,309 na urefu wa mita 185, eneo maalumu la meli lenye safu tano upande wa kaskazini na kusini, na jenereta 34 za turbo zenye uwezo wa pamoja wa kuzalisha umeme wenye nguvu ya kilowati milioni 22.5.

Tangu safu hizo maalum za meli zifunguliwe kwenye Bwawa la Magenge Matatu kwa usafirishaji wa majaribio mnamo Juni 2003, kiasi cha mizigo kinachopitia humo kimeongezeka kwa kasi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha