Ndege Kubwa C919 ya kwanza duniani kuundwa na China yafika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Meilan wa Haikou, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2023
Ndege Kubwa C919 ya kwanza duniani kuundwa na China yafika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Meilan wa Haikou, China
Ndege kubwa C919 iliyoundwa na China ikifika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Meilan huko Haikou, ikipita “mlango wa maji”, ambayo ni heshima ya juu zaidi kwa usafiri wa ndege ya abiria. Picha imetolewa na Uwanja wa Ndege wa Meilan.

Tarehe 2, Januari, saa 5:42 asubuhi (Saa za Beijing), ndege ya usafiri MU7807 ambayo ni ndege kubwa C919 ya kwanza duniani iliyoundwa na China na kumilikiwa na Shirika la Ndege la China Estern (CEAIR) imefika kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Meilan huko Haikou, kutoka Uwanja wa Ndege wa Hongqiao wa Shanghai, China. Ndege hiyo ilipita “mlango wa maji”, kuashiria heshima ya juu zaidi kwa usafiri wa ndege ya abiria, na kuanza rasmi kazi yake ya uthibitishwaji kwenye uwanja wa Haikou.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha