Sarafu na Stempu za Kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Sungura wa China zaanza kuuzwa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 06, 2023
Sarafu na Stempu za Kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa Sungura wa China zaanza kuuzwa
Tarehe 5, Januari, sarafu za kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China wa 2023 zinazotolewa na Benki Kuu ya China ilianza kuuzwa.

Mwaka Mpya wa Jadi wa Sungura unaoitwa pia kuwa mwaka wa Gui Mao kwa kalenda ya kilimo ya China unakaribia kuwadia. Tarehe 5 mwezi huu, sarafu za kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China wa 2023 zinazotolewa na Benki Kuu ya China ilianza kuuzwa, ambapo stempu maalumu ya “Mwaka wa Gui Mao” zilitolewa pia na Idara ya Posta ya China.

Kwenye upande wa mbele wa sarafu hiyo, kuna maneno ya lugha ya Kichina ya “Benki ya Umma ya China”, na “Yuan 10”, huku kwenye upande wa nyuma kukiwa na picha ya sungura ambayo inaonyesha sifa ya sanaa ya jadi ya ukataji wa karatasi ya China na mapambo ya mwaka mpya wa jadi.

Kila seti moja ya stempu maalum ya “Mwaka wa Gui Mao” ina stempu mbili, na picha kwenye stampu ni za sungura zilizochorwa na Huang Yongyu, msanii mzee mwenye umri wa karibu miaka 100.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha