Pilikapilika za usafiri wa mwaka mpya wa jadi wa China 2023 zaanza (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 13, 2023
Pilikapilika za usafiri wa mwaka mpya wa jadi wa China 2023 zaanza
Abiria akijaribu kufumbua fumbo kwenye taa ya kijadi katika ukumbi wa kusubiria treni wa Kituo cha treni cha Kusini cha Nanjing, China katika siku ya kwanza ya pilikapilika za usafiri wa mwaka mpya wa jadi wa China Tarehe 7, Januari 2023,. (Picha na Su Yang/People’s Daily)

Msimu wa usafiri wa mwaka mpya wa jadi wa China kwa kalenda ya kilimo ya China umerejea kwenye pilikapilika za kawaida. Pilikapilika hizo za Mwaka 2023 zitakuwa za siku 40 kuanzia Tarehe 7, Januari, hadi Tarehe 15, Februari.

Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ya China zinaonesha kuwa, inakadiriwa idadi ya jumla ya wasafiri wakati wa pilikapilika za usafiri wa mwaka mpya wa jadi wa China mwaka huu itakuwa bilioni 2.095 hivi, ambayo itaongezeka kwa asilimia 99.5 kuliko ile ya Mwaka 2022, na ni kurejea kwenye asilimia 70.3 ya idadi ya Mwaka 2019. Hali hiyo itahimiza matumizi ya nchini humu.

Inafahamika kwamba, vituo vingi vikuu vya treni vimetoa huduma mbalimbali mahsusi kwa abiria, huku vikitilia maanani ukingaji na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Korona na kufanya safari za kurudi nyumbani ziwe salama na za furaha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha