Uchomeleaji wa vyuma vyote vyenye urefu wa Mita 500 vya reli ya mwendo kasi ya Jakarta-Bandung wakamilika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 18, 2023
Uchomeleaji wa vyuma vyote vyenye urefu wa Mita 500 vya reli ya mwendo kasi ya Jakarta-Bandung wakamilika
Wafanyakazi wakifanya kazi kwenye hafla ya kukamilika kwa uchomeleaji wa vyuma vyote vyenye urefu wa mita 500 vinavyohitajika kwa ajili ya Reli ya Mwendokasi ya Jakarta-Bandung, huko Bandung, Indonesia, Januari 17, 2023. (Xinhua/Zulkarnain)

JAKARTA - Uchomeleaji wa vyuma vyote vyenye urefu wa mita 500 vinavyohitajika kwa ajili ya Reli ya Mwendokasi ya Jakarta-Bandung umekamilika siku ya Jumanne, na kuweka msingi imara wa kukamilisha kazi ya uwekaji njia za reli katikati ya Februari mwaka huu.

Jumla ya vipande 1,168 vya vyuma vya reli vyenye urefu wa mita 500 vinahitajika kwa njia hiyo ya reli yenye urefu wa kilomita 142.3, na kila kipande kimoja cha reli hiyo kimechomelewa kwa hatua 15 kutoka kwa vyuma vya reli vyenye urefu wa mita 50 vilivyoagizwa kutoka China. Kazi hiyo imekamilishwa kwa pamoja na wafanyakazi wa China na Indonesia.

Kampuni ya ujenzi ya China imetumia seti kamili ya vifaa vya kuchomelea reli ndefu vya China katika Kituo cha Kuchomelea Reli cha Tegualluar, ambacho ni kituo cha kwanza cha kuchomelea reli za mwendo kasi nje ya China. Kituo hicho kinachukua vifaa, teknolojia na viwango, na ubunifu wa China kukabiliana na hali joto ya juu na unyevu wa juu nchini Indonesia.

Njia hiyo ya reli ya mwendo kasi, ambayo ni mradi wa kihistoria chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja la China, unaunganisha mji mkuu wa Indonesia, Jakarta na mji wake wa nne kwa ukubwa wa Bandung, ambao pia ni mji mkuu wa Jimbo la Java Magharibi.

Ikiwa na muundo wa kasi ya kilomita 350 kwa saa, reli hiyo itapunguza muda wa usafiri kati ya Jakarta na Bandung kutoka zaidi ya saa tatu hadi dakika 40 hivi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha