China yatoa waraka kuhusu maendeleo ya kijani

(CRI Online) Januari 20, 2023

Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China imetoa waraka wa mpango wa maendeleo ya kijani wenye kichwa cha "Maendeleo ya Kijani ya China katika Zama Mpya."

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya kutolewa kwa waraka huo jana Alhamisi hapa Beijing, Naibu Mkurugenzi wa Kamati ya Maendeleo na Mageuzi ya Taifa ya China Zhao Chenxin amesema waraka huo umeeleza hatua na mafanikio ya China katika maendeleo ya kijani katika muongo mmoja uliopita, na kufafanua mawazo na uzoefu wa nchi hiyo kuhusu maendeleo ya kijani. Waraka huo umesema kijani ni sifa kuu ya China katika zama mpya, na maendeleo ya kijani yanatumika wakati China inaelekea maendeleo ya kisasa.

Takwimu zinaonesha kuwa kuanzia Mwaka 2012 hadi 2021, China ilipanda hekta milioni 64 za miti, kuzuia na kudhibiti hali ya jangwa zaidi ya hekta milioni 18.53 za ardhi, na kuongeza au kurejesha zaidi ya hekta laki 8 za ardhi oevu. Nishati mbadala imekuwa na nafasi muhimu zaidi katika mchanganyiko wa nishati nchini China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha