Mtaalam asema Ukuaji wa Uchumi wa China unasaidia ufufukaji wa uchumi wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 20, 2023
Mtaalam asema Ukuaji wa Uchumi wa China unasaidia ufufukaji wa uchumi wa Dunia
Picha hii iliyopigwa Januari 18, 2023 ikionyesha magari yakingoja kusafirishwa kwenye Bandari ya Yantai ya Mkoa wa Shandong nchini China. (Xinhua/Zhu Zheng)

BRUSSELS - China itatoa mchango muhimu katika kufufua uchumi wa Dunia baada ya janga la UVIKO-19, Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa China na Ubelgiji Bernard Dewit ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua katika mahojiano ya hivi karibuni.

Janga hilo limevuruga minyororo mingi ya ugavi wa kimataifa, na pia kuathiri uzalishaji, kupunguza usafiri, na kuleta wasiwasi mkubwa kote duniani. Hata hivyo, China ilipata ukuaji mzuri wakati wa janga hilo, na imekuwa nchi ya pili duniani kwa kuwa na uchumi mkubwa, Dewit amesema.

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) lilikadiria mwezi Novemba uliopita kwamba ongezeko la uchumi wa China litafikia asilimia 4.4 Mwaka 2023. Kutokana na hali hiyo, Dewit amesema, China itaendelea kutoa usaidizi muhimu kwa viwanda na minyororo ya ugavi ya kimataifa ili kurejea katika shughuli zake za kawaida.

China pia ni mhusika mkuu katika minyororo ya thamani ya kimataifa, Dewit amesema, na kwa hivyo ina athari kubwa katika utengenezaji wa bidhaa, usafirishaji na ugavi wa kimataifa.

Dewit amesema China imeweza kufufuka vyema kutokana na athari za janga la UVIKO-19, shukrani kwa sehemu juu ya hatua kali za kichocheo za serikali na hatua madhubuti za kudhibiti janga.

Sera za mageuzi ya uchumi na kufungua mlango zinazoendelea kutekelezwa nchini China, pamoja na kuongezeka kwa kundi kubwa la watu wenye mapato ya kati na kuongezeka kwa matumizi ya nchi hiyo, vyote vinatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi.

Kwa ujumla, ingawa kunaweza kuwa na kutokuwa na uhakika katika muda mfupi, mtazamo wa uchumi wa muda mrefu wa China kwa ujumla unachukuliwa kuwa mzuri, amebainisha.

Kwa kuwa China ni mdau mkuu wa uchumi wa Dunia, na mtumiaji mkubwa wa bidhaa na huduma, uchumi wa China wenye nguvu unaoendelea kwa hatua madhubuti utasaidia uchumi wa dunia nzima, Dewit ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha