Xi Jinping atuma salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa Wachina wote, akiwataka kufanya kazi kwa bidii ili kujenga siku nzuri za baadaye (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 22, 2023
Xi Jinping atuma salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa Wachina wote, akiwataka kufanya kazi kwa bidii  ili kujenga siku nzuri za baadaye
Viongozi wa Chama na Serikali ya China Xi Jinping, Li Keqiang, Li Zhanshu, Wang Yang, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Han Zheng, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Wang Qishan wakishiriki kwenye sherehe ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China Januari 20, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Baraza la Serikali la China, ametuma salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa wachina wote siku ya Ijumaa kwenye sherehe ya mwaka huu mpya wa Sungura wa 2023 iliyofanyika Beijing, Mji Mkuu wa China.

Xi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ametoa hotuba katika mkusanyiko kwenye Jumba la Mikutano ya Umma, akituma salamu kwa Wachina wa makabila yote, ndugu wa Hong Kong, Macao na Taiwan, na Wachina wanaoishi katika sehemu mbalimbali duniani.

Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa Kalenda ya Kilimo ya China, imeangukia leo Januari 22.

Mwaka uliomalizika wa Chuimilia ni mwaka muhimu sana katika historia ya Chama na nchi, Rais Xi amesema.

Kutokana na kukabiliwa na upepo mkali na mawimbi katika hali ya kimataifa na changamoto za kazi za kutafuta mageuzi na maendeleo na kuhakikisha utulivu nchini China, Chama kizima, jeshi zima na watu wa makabila yote wa China wamekabiliana na changamoto hizo, kushikamana kwa karibu na kufanya kazi kwa bidii, kuandika ukurasa mpya wa maendeleo ya kijamaa, amesema.

Li Keqiang aliongoza sherehe hiyo. Li Zhanshu, Wang Yang, Li Qiang, Zhao Leji, Wang Huning, Han Zheng, Cai Qi, Ding Xuexiang, Li Xi na Wang Qishan pia walishiri kwenye sehere hiyo.

Katika mwaka uliopita, CPC iliandaa kwa mafanikio Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, Rais Xi amebainisha, na kupongeza juhudi za China katika kuharakisha ujenzi wa muundo mpya wa maendeleo, kukuza maendeleo ya kiwango cha juu, kudumisha ongezeko la uchumi, kupata mavuno mengi, kudumisha utulivu wa jumla wa ajira na bei, na kuhakikisha maisha mazuri ya watu.

Pia amepongeza hatua iliyofikiwa katika uimarishaji wa matokeo ya kuondokana na umaskini, mafanikio ya kiteknolojia na uboreshaji wa ikolojia.

Rais Xi ametaja mafanikio mbalimbali ya China ikiwa ni pamoja na kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi, Kuimarisha Mawasiliano ya kindugu kwenye Mlango Bahari wa Taiwan, kulinda maisha ya watu dhidi ya janga la UVIKO-19, kuandaa kwa mafanikio Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC na kuimarisha amani, mshikamano na utulivu wa nchi.

Huku akisema mwaka huu ni mwaka wa kwanza wa kuanza kutekeleza mipango na maazimio ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, Rais Xi ametaka kufanya juhudi kubwa zaidi katika kukabiliana na UVIKO-19 na kutafuta maendeleo ya kisasa ya China katika zama mpya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha