Wacheza “Dragon kuu ya Luoshan” wa Nanjing watembea kijijini ili kutakia heri na baraka (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 28, 2023
Wacheza “Dragon kuu ya Luoshan” wa Nanjing watembea kijijini ili kutakia heri na baraka

Tarehe 26, Januari, wacheza “Dragon Kuu ya Luoshan” walitembea kijijini Luoshan kilichopo pembezoni mwa Ziwa Shijiu, katika Mji wa Nanjing, China, dragon hiyo ikiinua kichwa chake kwa kuwatakia heri na baraka wanavijiji. Sanaa hii ya Dragon ina umbo mkubwa, ikiwa na urefu wa karibu mita 100. Shughuli ya kutembea na Dragon ya Luoshan ilianzishwa wakati wa enzi ya Ming ya China, na hadi hivi sasa historia yake imezidi miaka 400, na imekuwa ya urithi wa utamaduni usioshikika wa kitaifa wa China. Picha hii ikionesha wanavijiji wakiwa wameibeba dragon kuu ya Luoshan na kucheza ngoma. (Picha imepigwa na Yangbo/Chinanews)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha