

Lugha Nyingine
Kikosi cha uokoaji cha China chaelekea Uturuki (6)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 08, 2023
![]() |
Picha hii iliyopigwa kwa simu ya mkononi ikionyesha wafanyakazi wa kikosi cha uokoaji cha China wakipanda ndege maalum katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Februari 7, 2023. (Xinhua/Wu Siyu) |
Kikosi cha uokoaji cha China kimeondoka Beijing kuelekea Uturuki kwa ndege maalumu Jumanne alasiri ili kujiunga na juhudi za usaidizi kutokana na kutokea kwa tetemeko kubwa la ardhi nchini humo.
Kikosi hicho chenye watu 82 kimetumwa na Wizara ya Usimamizi wa Dharura ya China, kwa ombi la Serikali ya Uturuki.
Kikosi hicho, kinachoundwa na watu wa kikosi cha zima moto na uokoaji cha Beijing, watu wa Idara ya kitaifa ya Kukabiliana na Tetemeko la Ardhi na Hospitali Kuu ya Dharura ya Beijing, kimebeba zana na vifaa vya uokoaji.
Takriban watu zaidi ya 6,000 wameuawa hadi kufikia Jumanne alasiri na makumi ya maelfu ya watu kujeruhiwa baada ya tetemeko hilo kubwa la ardhi kukumba maeneo ya Uturuki na nchi jirani ya Syria siku ya Jumatatu.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma