Watoto wa Namibia waeleza hisia zao kupitia vipindi vya redio wanavyovitayarisha wenyewe

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 14, 2023
Watoto wa Namibia waeleza hisia zao kupitia vipindi vya redio wanavyovitayarisha wenyewe
Mathew Haipare (kushoto) akipozi ili kupigwa picha pamoja na mama yake (kati) na Elizabeth Hamurenge, mratibu wa studio huko Windhoek, Namibia, Februari 13, 2023. (Picha na Ndalimpinga Iita/Xinhua)

WINDHOEK - Kundi la watoto wa Namibia Jumatatu walirekodi vipindi vya sauti ambavyo vitarushwa kwenye redio ya Shirika la Utangazaji la kitaifa la Namibia.

Mathew Haipare, 13, pamoja na wenzake, wamezungumza mawazo yao kuhusu masuala ya kijamii yanayowakabili sana watoto kwenye studio, inayojulikana kwa jina la Uitani Childline Radio, huko Windhoek, Mji Mkuu wa Nambia.

Ikiwa ni chimbuko la Shirika la Lifeline Childline la Namibia, asasi ya kiraia inayotoa ushauri nasaha bila malipo kwa wenyeji, studio hiyo ilizinduliwa Mwaka 2005 ili kuruhusu watoto kuwasilisha ujumbe wao wenyewe kwa kuleta mchango mkubwa.

Vipindi hivyo vyenye maudhui hayo hutayarishwa kutoka kwenye studio na huchukua dakika 30 hadi saa moja kwa kila kipindi, hurekodiwa kwanza na baadaye kurushwa kwenye redio ya Shirika la Utangazaji la Namibia na kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii.

Stanley Similo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Namibia, amesema kipindi hicho cha watoto kinatangazwa kila Jumamosi asubuhi na kimekua na kuwa kituo maarufu kwa watoto wa Namibia wanaotaka kufahamishwa kuhusu haki zao.

"Kimewafikia watoto katika maeneo ya vijijini, na mchango wake haupimiki," amesema.

Takriban watoto 20 kwa sasa akiwemo Mathew Haipare wanafanya kazi na studio hiyo wakiwa ni watangazaji na waandaaji wa vipindi, amesema Elizabeth Hamurenge, mratibu wa studio hiyo, ambaye huwaongoza watangazaji hao wachanga, na kusimamia ubora wa vipindi.

"Nilitaka kujiunga na studio hii kwa sababu nimekuwa nikijaribu kuwasaidia watoto wasio na makazi. Nilitaka kutumia sauti yangu kuwa sauti yao," anasema Haipare, ambaye alijiunga na studio hiyo Februari 2022.

Studio hiyo imeendelezwa kwa ufadhili wa Lifeline Childline, wafadhili na washirika wakuu, amesema Hamurenge ambaye ni mratibu wa studio hiyo, na studio iko mbioni kuomba leseni ya utangazaji ili kuwa kituo cha kujitegemea na cha moja kwa moja, hivyo kuwezesha zaidi. mwingiliano thabiti wa watoto na kuleta mchango kwa watoto ambao wanakabiliwa na changamoto katika jamii zao. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha