

Lugha Nyingine
Shule kote nchini zarejea uchangamfu wake wa awali wakati wa muhula mpya wa masomo wa Majira ya Mchipuko (2)
BEIJING- Takriban walimu na wanafunzi milioni 300 wamerejea katika maeneo ya shule kote nchini China, wakati ambapo muhula mpya wa masomo wa majira ya mchipuko ukianza kwa njia tofautitofauti katika maeneo ya ngazi ya mkoa.
Muhula huu mpya wa masomo ni muhula wa kwanza baada ya China kupunguza masharti ya udhibiti wa janga la UVIKO-19 kutoka Daraja A hadi Daraja la B mnamo Januari 8. Naibu Waziri Mkuu wa China, Sun Chunlan Februari 6 alihimiza kufanyika juhudi za kuboresha usimamizi wa shule kulingana na hatua za kitaifa za kudhibiti UVIKO-19 na kurejesha kikamilifu hali ya kawaida katika shughuli za masomo mashuleni.
Siku ya Jumatatu, zaidi ya wanafunzi milioni 1 wa shule za msingi na sekondari mjini Beijing walirejea shuleni.
Katika miaka mitatu iliyopita, kutokana na wasiwasi wa usalama wa afya katika mapambano dhidi ya janga hilo nchini China, mara kwa mara wanafunzi walibaki nyumbani mwao na kuhudhuria masomo yao kupitia njia ya kuongozwa mtandaoni.
Ma Luo, Mkurugenzi wa Kituo cha Michezo cha Wanafunzi katika Shule ya Sekondari ya Guangqumen katika Eneo la Dongcheng la Beijing, anasema madarasa ya Elimu ya Michezo (PE) kwa muhula huu yatatilia mkazo katika kuwasaidia wanafunzi "hatua kwa hatua kurejesha nguvu zao za kimwili huku mazoezi ya utimamu wa mwili na michezo ya mpira vikianza kwanza badala ya kukimbia."
Kutokana na kupunguzwa kwa kiasi kikubwa kwa masharti ya kudhibiti janga la korona, maeneo ya shule sasa hayahitaji tena majibu ya vipimo yanayoonesha kutokuwa na maambukizi ya UVIKO-19 ili kuingia.
Kwa mujibu wa maagizo ya Wizara ya Elimu ya China, wanafunzi wanatakiwa kuripoti halijoto ya mwili wao kabla ya kurejea shuleni. Na kama wakihisi kuwa na dalili kama vile homa, wanatakiwa kuripoti hali hiyo kweli na kuchelewesha kurejea kwao shuleni huku wakisubiri kuthibitisha hali ya maambukizi ya UVIKO-19.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma