Habari picha ya muuzaji wa maua moja kwa moja mtandaoni katika Mkoa Yunnan wa China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 15, 2023
Habari picha ya muuzaji wa maua moja kwa moja mtandaoni katika Mkoa Yunnan wa China
Picha hii iliyopigwa Februari 12, 2013 ikimwonyesha Bi Xixi akihamisha maua mabichi ili yafungashwe kwenye shamba lake la maua huko Qujing, Mkoa wa Yunnan, Kusini Magharibi mwa China, Februari 12, 2023. (Xinhua/Jiang Wenyao)

Soko la Maua la Dounan huko Kunming, Mkoa wa Yunnan wa China ndilo soko kubwa zaidi la biashara ya maua mabichi yaliyokatwa barani Asia. Kila siku usiku unapoingia, mfanyabiashara ya maua Bi Xixi huingia kwenye pilikapilika na shughuli za biashara ya maua hapa.

Ukiacha kazi ya kupanda na kuzalisha maua, Bi pia ni mtangazaji wa moja kwa moja wa mtandaoni. Miaka mitatu iliyopita, alipokuwa akipalilia mashamba yake ya maua, Bi alifungua bila kutarajiwa programu ya kutangaza moja kwa moja mtandaoni kwenye simu yake. Kwa mshangao, kipindi chake cha kutangaza kazi yake moja kwa moja mtandaoni si tu kilipata idadi kubwa ya wafuasi, lakini pia kilimpa wazo la kuuza maua mabichi yaliyokatwa.

Tofauti na wauzaji wengi wa moja kwa moja mtandaoni wanaolenga mauzo, Bi Xixi hujifanya zaidi kama mwongoza watalii, akiwapelekea watazamaji wake wa mtandaoni kutoka kwenye shamba la maua hadi kwenye soko la maua na kushiriki nao habari za maua.

Katika Soko la Maua la Dounan, ambalo mara nyingi hujulikana kama mji mkuu wa maua wa Asia, wachuuzi wa kawaida wa maua wamejizoesha kwa muda mrefu na wauzaji wa moja kwa moja mtandaoni kama Bi huyo na aina ya biashara yao. Wanafahamu kikamilifu kwamba maelfu ya wapenzi wa maua wanaweza kuwa wakitazama mtandaoni moja kwa moja kutokea sokoni hapo kupitia simu janja. (Xinhua/Jiang Wenyao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha