Uhamishaji wa samaki pomboo wasio na mapezi wa Ziwa Poyang (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 17, 2023
Uhamishaji wa samaki pomboo wasio na mapezi wa Ziwa Poyang
Wafanyakazi wakiwazingira samaki pomboo wasio na mapezi kwa boti za mwendo kasi na meli za uvuvi kwenye pwani ya eneo la maji la Songmenshan katika Ziwa Poyang, Mkoa wa Jiangxi, China. (Picha imepigwa kwa droni Tarehe 15,Februari).

Samaki Pomboo wasio na mapezi ni spishi bora zaidi na alama ya ulinzi wa viumbe majini wa Mto Changjiang, na ni viumbe ambao wako hatarini sana kutoweka.

Ili kupunguza hatari za kukwama kwa samaki pomboo wasio na mapezi na uhaba wa chakula, na kuhimiza uboreshaji wa muundo wa viumbe majini wa eneo la Mto Changjiang, siku hizi Idara ya kilimo na vijiji ya Mkoa wa Jiangxi wa China na Idara ya utafiti wa viumbe wa majini ya Taasisi ya Sayansi ya China pamoja na idara nyingine kwa pamoja zilifanya kampeni ya uhamishaji na ulinzi wa samaki pomboo wasio na mapezi wa Mto Changjiang kwenye eneo la maji la Songmenshan katika Ziwa Poyang, Mkoa wa Jiangxi. Baada ya siku tatu za kuwazingira na kuwakamata, kuwafanyia upimaji wa afya, kuwalinda na kuwasafirisha, idara husika kwa pamoja zilihamisha samaki pomboo wasio na mapezi wawili wa kiume kwenye eneo la maji ya Bandari ya Kusini na Kaskazini ya Ziwa Poyang katika Wilaya ya Hukou, Mkoa wa Jiangxi. Waandishi wa habari walirekodi mchakato mzima wa uhamishaji wa pomboo hao wasio na mapezi kwenye "nyumba yao mpya" .

(Picha na Wanxiang/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha