

Lugha Nyingine
Magari ya kuruka yanatarajiwa kuruka kwa urahisi angani katika mji
XPENG AEROHT ni kampuni inayoshika nafasi ya mbele nchini China kwenye sekta ya viwanda vya kuunda magari yanayotumia nishati ya umeme yenye teknolojia za akili bandia, na pia ni kampuni kubwa zaidi ya kuunda magari ya kuruka barani Asia. Gari XPENG X2 la kampuni hiyo limepata kibali maalumu cha urukaji kutoka Idara ya Usimamizi wa Safari ya Anga ya Abiria ya eneo la Kusini Kati la China.
XPENG X2 linaweza kubeba abiria wawili, na ukomo wa uzito linaoweza kubeba ni kilogramu 200. Kasi yake ya juu zaidi ya kuruka ni kilomita 130 kwa saa. XPENG X2 litafaa kutumika kwa kuruka kwenye anga ya chini katika miji ya siku za baadaye, na pia litaweza kuhudumia katika shughuli kama vile za utalii, uokoaji nje ya miji, na usafirishaji kwa ajili ya matibabu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma