Ndege karibu elfu kumi wapita majira ya baridi kwenye ardhi oevu ya Jiangsu, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 22, 2023
Ndege karibu elfu kumi wapita majira ya baridi kwenye ardhi oevu ya Jiangsu, China

Tarehe 19, Februari, 2023, ndege wa avocet karibu elfu kumi walitua ili kucheza na kutafuta chakula kwenye ardhi oevu karibu na mlango wa Mto Honghe huko Lianyungang, Mkoa wa Jiangsu wa China. Imeelezwa kuwa, eneo la Liangyun la Mji wa Lianyungang lina maliasili bora za pwani, na ni sehemu muhimu zilizo karibu na bahari kwa viumbe hai kuishi na kuzaliana, na pia ni kituo cha mapumziko kwa ndege wanapohama. Eneo hilo limekuwa likiwavutia ndege wa avocet kupita huko wakati wa majira ya baridi kwa miaka mingi mfululizo. (Picha/CFP)

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha