Bunge la Umma la China laanza mkutano wa kamati ya kudumu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 24, 2023
Bunge la Umma la China laanza mkutano wa kamati ya kudumu
Li Zhanshu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China (NPC), akiongoza kikao cha kwanza cha mkutano wa 39 wa wajumbe wote wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la 13 la China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, China, Februari 23, 2023 (Xinhua/Zhang Ling)

BEIJING - Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la 13 la China (NPC), imeanza mkutano wake wa 39 Alhamisi wa kufanya maandalizi kwa ajili ya mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China, utakaofunguliwa Machi 5.

Li Zhanshu, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China , ameongoza kikao hicho cha kwanza cha mkutano huo wa 39. Jumla ya wajumbe 162 wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Umma la China walihudhuria mkutano huo.

Wajumbe walipitia rasimu ya uamuzi wa kurekebisha matumizi ya baadhi ya vifungu vya Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwa jeshi wakati wa vita.

Katika maandalizi kwa ajili ya mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China, wajumbe walijadili rasimu ya ripoti ya kazi ya Kamati ya Kudumu ya NPC, rasimu ya ajenda ya mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14, rasimu ya orodha ya majina ya wajumbe na makatibu wakuu, na rasimu ya orodha ya majina ya wajumbe waalikwa wasiopiga kura kwenye mkutano.

Wajumbe waliohudhuria mkutano pia walisikia ripoti ya uchaguzi wa wajumbe wa Bunge la Umma la 14 la China iliyotolewa na Yang Zhenwu, Katibu Mkuu wa Kamati ya Kudumu ya NPC.

Ripoti hiyo imesema, Jumla ya wajumbe 2,977 wa Bunge la Umma la 14 la China wamechaguliwa, na wanawakilisha kwa upana jamii na kada zote za Wachina. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha