Kampuni za China na Saudi Arabia zafungua kiwanda cha kuunganisha mabasi nchini Misri

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 02, 2023
Kampuni za China na Saudi Arabia zafungua kiwanda cha kuunganisha  mabasi nchini Misri
Picha iliyopigwa Februari 28, 2023 ikionyesha mabasi kwenye kiwanda cha kuunganisha mabasi kilichojengwa kwa pamoja na kampuni za China na Saudia katika Jimbo la Suez, Misri. Kiwanda kipya cha kuunganisha mabasi kilichojengwa kwa pamoja na kampuni za China na Saudi kimeanza uzalishaji katika Mji wa New Suez, huku kundi la kwanza la mabasi ya usafiri yakitarajiwa kundwa tayari hivi karibuni. (Xinhua/Ahmed Gomaa)

CAIRO - Kiwanda kipya cha kuunganisha mabasi kilichojengwa kwa pamoja na kampuni za China na Saudi kimeanza uzalishaji katika Mji wa New Suez, huku kundi la kwanza la mabasi ya usafiri yakitarajiwa kuanza kuunganishwa sehemu zake na kukamilika hivi karibuni.

Akizungumza kwenye uzinduzi uliofanyika mjini humo siku ya Jumanne, mwenyekiti wa kampuni ya Saudi ya ATM Misr, Hamed Al Mutabagani, amesema kiwanda hicho kimesanifiwa kwa kuwa na uwezo wa kuunda mabasi 500 kwa mwaka.

"Kiwanda hiki kinachukua eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 164,000 na kina vifaa vya kisasa vya uzalishaji, ghala, na vifaa vya kudhibiti ubora,” ameongeza kusema Al Mutabagani, ambaye kampuni yake imejenga kiwanda hicho kwa pamoja na kampuni ya uundaji mabasi ya China, King Long.

ATM Misr imewekeza pauni bilioni 1 za Misri (kama dola milioni 3.3 za Kimarekani) katika kujenga kiwanda hicho, huku King Long imetoa teknolojia na vifaa kamili vya magari.

Kwa mujibu wa makubaliano ya ushirikiano, kiwanda hicho kitaipatia kampuni ya biashara ya usafiri wa mabasi ya Saudia ya National Trade mabasi 51 yaliyokamilika, 26 kati ya mabasi hayo yatatumia sehemu za gari zinazotolewa na King Long.

"Takriban asilimia 60 ya uundaji wa mabasi unatumia vifaa vinavyotengenezwa nchini Misri, katika jitihada za kusaidia kuwekeza viwanda vya magari nchini Misri,” amesema Al Mutabagani, na kuongeza kuwa nchi za Ghuba ni soko linalolengwa na kiwanda hicho.

Inatarajiwa kuwa kiwanda hicho kitatumia faida ya eneo lake lililo karibu na bandari tatu muhimu kufikia masoko ya Afrika na Ulaya, ameeleza.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha