

Lugha Nyingine
Mji wa Moscow Russia wafungua njia ndefu zaidi ya reli ya chini ya ardhi duniani (2)
![]() |
Mwanamke akitazama ramani ya njia ya reli ya Big Circle huko Moscow, Russia, Machi 1, 2023. (Picha na Alexander Zemlianichenko Jr/Xinhua) |
MOSCOW - Mji wa Moscow nchini Russia siku ya Jumatano umefungua njia ya reli yenye urefu wa kilomita 70 ya Big Circle Line (BCL), ambayo ni njia ya reli ndefu zaidi ya chini ya ardhi duniani.
Njia hiyo ya treni za chini ya ardhi imejengwa kuanzia Mwaka 2011 hadi 2022. Sehemu ya kwanza ya BCL ilifunguliwa Mwaka 2018, na sehemu nyingine yenye urefu wa kilomita 20, ambayo ni ndefu zaidi katika historia ya treni za chini ya ardhi ya mji huo mkuu wa Russia, ilizinduliwa Desemba 2021.
BCL ina stesheni 31, na 24 kati ya hizo zinatoa njia 47 za kubadilishana treni kwa njia zilizopo sasa na zitakazojengwa hapo baadaye za treni za chini ya ardhi.
Maksim Liksutov, Naibu Meya wa Mji wa Moscow anayeshughulikia mambo ya usafiri, amesema kuwa BCL itatumika kama kichocheo cha maendeleo ya mji huo mkuu kwa miongo kadhaa ijayo, na kuongeza kuwa itasaidia kupunguza msongamano wa magari barabarani kwenye barabara kuu za mji huo kwa asilimia 15, na itapunguza msongamano kwenye njia za treni za chini ya ardhi kwa asilimia 25.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma