

Lugha Nyingine
Mjumbe wa Bunge la Umma la China: Siku za furaha bado zinakuja
Kwenye mjadala wa wajumbe wa Mkoa wa Henan wa Bunge la Umma la 13 la China, Li Liancheng ambaye ni mjumbe wa Bunge la 13 la Umma la China akiwakilisha kijiji chake cha Xixinzhuang aliripoti ndoto nane za wakulima kwa Katibu Mkuu wa Chama Xi Jinping.
"Wakulima wa China wana ndoto nane. Waache watoto wao waende shule nzuri karibu, watafute hospitali nzuri ya kuonana na daktari, watafute ajira karibu na vijiji vyao, wasiende maeneo ya mbali kutafuta kazi, wawe na mazingira mazuri ya ikolojia kijijini, na washiriki na kufanikisha ustawi wa vijiji..."
Xi Jinping alitabasamu na kusema: "Ulichosema leo ni mahitaji ya wakulima wengi kwa maisha ya furaha ... Madhumuni yetu ni kuwatumikia watu na kufanya juhudi kwa vitendo kufuatia matarajio ya watu juu ya maisha ya furaha."
Baada ya kurejea katika kijiji chake baada ya mikutano miwili ya China, Li Liancheng aliwaambia wanakijiji kile ambacho Xi Jinping alisema kwa ukamilifu, ambacho kilimtia moyo kila mtu.
Kwa miaka mingi, Kijiji cha Xixinzhuang kimebadilika sana. "Ndoto zinatimizwa moja baada ya nyingine." Li Liancheng amewaambia waandishi wa habari kwa furaha:
Kwa ndoto ya kusoma, kuna shule za chekechea na za msingi katika kijiji hicho, zinazovutia zaidi ya wanafunzi 1,300 kutoka eneo la jirani kwenda shule;
Kwa ndoto ya afya, hospitali yenye vitanda zaidi ya 500 kijijini itajengwa na kuanza kutumika mwaka huu;
Aidha ndoto nyingine zikiwemo za ajira na utunzaji mazingira nazo zinatimia kwa mipango na utekelezaji.
Li Liancheng amechaguliwa tena kuwa mjumbe wa Bunge la Umma la 14 la China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma