China yalenga ukuaji wa haraka wa uchumi na wenye ubora wa juu wakati wa kuhimiza ufufukaji wa uchumi na ujenzi wa mambo ya kisasa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 06, 2023
China yalenga ukuaji wa haraka wa uchumi na wenye ubora wa juu wakati wa kuhimiza ufufukaji wa uchumi na ujenzi wa mambo ya kisasa
Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) ukifunguliwa kwenye Jumba la Mikutano ya Umma hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 5, 2023. (Xinhua/Yue Yuewei)

BEIJING - China inalenga kufikia ukuaji wenye kasi wa uchumi wa karibu asilimia 5 na maendeleo yenye ubora wa juu Mwaka 2023, wakati nchi hiyo yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani ikikusanya nguvu ili kufuata mwelekeo wa ufufukaji wa uchumi na kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa.

Lengo hilo la ukuaji wa uchumi lililowekwa, ambalo ni la juu zaidi ya ukuaji wa asilimia 3 uliorekodiwa katika Pato la Taifa (GDP) mwaka jana, ni moja ya malengo muhimu ya maendeleo yaliyoainishwa kwenye ripoti ya kazi ya serikali iliyotolewa na Waziri Mkuu wa China, Li Keqiang kwa Buge la Umma la 14 la China, ambalo limeanza mkutano wake wa kila mwaka jana Jumapili.

Lengo la ukuaji wa takriban asilimia 5 "ni muhimu ili kuhakikisha uthabiti na utulivu katika ukuaji wa uchumi, ajira na bei," Ripoti nyingine ya Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China (NDRC) juu ya utekelezaji wa mpango wa Mwaka 2022 wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii na juu ya rasimu ya mpango wa Mwaka 2023 wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

"Kwa China, Mwaka 2023 ni mwaka wa kurejea kukua kwa kasi kwa uchumi," Liu Shouying, Mkuu wa Chuo cha Uchumi katika Chuo Kikuu cha Umma cha China amesema.

Kurejesha ukuaji wa Uchumi

Uchumi wa China unaendelea kuimarika, huku kukiwa na kuongeza mahitaji ya matumizi, usambazaji kwenye soko, uzalishaji kwenye viwanda na matarajio ya biashara, Waziri Mkuu Li amesema huku akiweka bayana kuwa uchumi wa China unaonyesha uwezo na faida kubwa ya kuimarika na kasi ya ukuaji zaidi.

Mwaka huu, China inalenga kuongeza nafasi mpya za ajira milioni 12 mijini, na kudhibiti ukosefu wa ajira uliochunguzwa mijini kwa asilimia 5.5 hivi. Na upandaji wa bei ya wanunuzi utadhibitiwa kwenye kiwango cha asilimia 3, na kuuwezesha uzalishaji wa nafaka uzidi tani milioni 650.

Ubora wa maendeleo ni muhimi zaidi

Wakati ikiweka juhudi kubwa zaidi kwenye ukuaji wa uchumi, Serikali ya China haitatafuta ukuaji wa uchumi bila kujali gharama yoyote. Badala yake, inataka uchumi wenye kutilia maanani kulinda mazingira na mabadiliko ya tabia nchi na yenye ufanisi zaidi.

Wakati akitoa ripoti ya kazi ya serikali, Waziri Mkuu Li kwa mara nyingine amesisitiza juhudi za kutafuta maendeleo yenye ubora wa juu, akielezea vipaumbele vya sera kama vile kuharakisha ujenzi wa kisasa wa mfumo wa viwanda na kuhimiza kazi ya kubadilisha muundo wa maendeleo ya kijani.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha