

Lugha Nyingine
Mavuno ya Viazi Mviringo yapatikana kwenye Mashamba makubwa mkoani Yunnan, China (3)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 07, 2023
![]() |
Picha iliyopigwa kutoka juu ikionesha mashamba ya viazi mviringo kwenye Wilaya ya Yun ya Mkoa wa Yunnan, China. (Picha/Yuan Lingfeng) |
Siku hizi, mavuno ya viazi mviringo yamepatikana kwenye mashamba ya zaidi ya hekta 670 katika Wilaya ya Yun ya Mkoa wa Yunnan, China.
Katibu wa tawi la Chama cha Kikomunisti cha China la Kijiji cha Shuimo, ambaye pia ni mkurugenzi wa Kamati ya Wanakijiji wa Duan Xuelan alijulisha kuwa, viazi mviringo vinavyopandwa kwenye mashamba ya kijiji hicho ni vikubwa, vya ubora na havijaliwa na wadudu. Kwa wastani mazao ya viazi ya kila mu (takriban 0.067 hekta) yanafikia tani 3.8, na viazi vya kila tani vinauzwa kwa bei zaidi ya Yuan 2600 (takriban Shilingi za Tanzania laki 8.74). Mapato ya mwaka ya wanakijiji wote kutokana na upandaji viazi mviringo yamezidi Yuan milioni 11 (takriban Shilingi za Tanzania bilioni 3.70).
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma