Rekodi mpya! Uundaji wa Meli kubwa zaidi ya kontena duniani wakamilika Shanghai

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 10, 2023
Rekodi mpya! Uundaji wa Meli kubwa zaidi ya kontena duniani  wakamilika Shanghai
Meli kubwa zaidi ya kontena duniani iliyoundwa huko Shanghai.(Mpiga picha:Zhang Li)

Tarehe 9, Machi, uundaji wa meli ya kontena inayoweza kubeba makontena 24116 iliyoundwa na Hudong Zhonghua, Kampuni tanzu ya Shirika la Uundaji Meli la China umekamilika kwenye Kituo cha uundaji wa meli cha Changxing cha Shirika la Uundaji Meli la China. Hii ni meli kubwa zaidi iliyoundwa na kukamilika duniani, ambayo imevunja rekodi ya “Meli ya Changyi” iliyokamilika Mwezi Juni, Mwaka 2022 yenye uwezo wa kubeba makontena 24000.

Meli hii imesanifiwa kwa kujitegemea na Kampuni ya Hudong Zhonghua. Ina urefu wa jumla wa mita 399.99, upana wake ni mita 61.5 na kimo chake ni mita 33.2. Inaweza kubeba makontena kwenye ngazi 25, ambazo ni sawa na urefu wa jengo lenye ghorofa 22, na inaweza kubeba mizigo ya tani zaidi ya 240,000, Meli hiyo inaweza kubeba makontena 24116 yenye kipimo cha kawaida, na inastahili haswa kuwa meli kubwa zaidi na inayobeba makontena mengi zaidi kwenye bahari kuliko meli nyingine zote kwa hivi sasa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha