Ripoti ya kazi ya serikali ya China na nyaraka nyingine zapitishwa leo Jumatatu kwenye Mkutano wa Bunge la Umma la 14 la China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 13, 2023
Ripoti ya kazi ya serikali ya China na nyaraka nyingine zapitishwa leo Jumatatu kwenye Mkutano wa Bunge la Umma la 14 la China
Zhao Leji, Mjumbe wa kudumu wa Tume Tendaji ya Wenyeviti ya mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC), akiongoza mkutano wa tisa wa tume hiyo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Machi 12, 2023. (Xinhua/Xie Huanchi)

BEIJING – Bunge la Umma la 14 la China limepitisha nyaraka kadhaa muhimu kwenye mkutano wa wajumbe wote uliofanyika leo Jumatatu.

Uamuzi huo wa kuwasilisha nyaraka hizo kwenye Bunge la Umma la 14 la China ulitolewa kwenye mkutano wa tisa wa Tume Tendaji ya Wenyeviti ya Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China uliofanyika Jumapili alasiri, ukiongozwa na Zhao Leji, mjumbe wa kudumu wa tume hiyo.

Nyaraka hizo zinajumuisha rasimu ya maazimio ya ripoti ya kazi ya serikali, kuhusu utekelezaji wa mpango wa kitaifa wa China wa maendeleo ya uchumi na jamii wa Mwaka 2022 na mpango wa Mwaka 2023, na utekelezaji wa bajeti kuu na za serikali za mitaa Mwaka 2022 na bajeti ya Mwaka 2023.

Rasimu ya maazimio ya ripoti za kazi za Kamati ya Kudumu ya 13 ya Bunge la Umma la China (NPC), Mahakama ya Kuu ya Umma ya China na Idara ya Mashtaka ya Umma ya China pia zitapigiwa kura.

Kabla ya mkutano huo, Tume Tendaji ya Wenyeviti ilifanya mkutano wake wa saba, ambao pia uliongozwa na Zhao.

Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) umekamilika leo Jumatatu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha