Rais Xi Jinping asisitiza juhudi za ujenzi wa nchi yenye nguvu na ustawi wa taifa

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2023
Rais Xi Jinping asisitiza juhudi za ujenzi wa nchi yenye nguvu na ustawi wa taifa
Rais Xi Jinping na viongozi wengine wa China wakihudhuria kikao cha kufunga Mkutano wa Kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China (NPC) kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 13, 2023. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumatatu alipotoa hotuba kwenye kikao cha ufungaji wa mkutano wa kwanza wa Bunge la Umma la 14 la China alitoa wito wa kuunda nguvu kubwa kwa ajili ya kujenga nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa na kuendeleza ustawishaji wa Taifa la China wakati mapazia ya "mikutano mikuu miwili" ya kila mwaka ya China yakifungwa, ambayo imefungua ukurasa mpya wa maendeleo ya kisasa ya China kwa kuchagua viongozi wapya wenye uwezo na kupitisha sera mpya katika sekta zote.

Rais Xi amesema, “Kuanzia siku hii na kuendelea hadi katikati ya Karne ya 21, kazi kuu ya Chama kizima cha Kikomunisti cha China (CPC) na watu wote wa China itakuwa ni kuijenga China kuwa nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa kwa pande zote na kuendeleza ustawishaji wa Taifa la China katika sekta zote” .

Rais Xi ameahidi kutekeleza wajibu wake kwa umakini mkubwa, kufanya kila awezalo, na kuthibitisha kuwa anastahili kuaminiwa na wajumbe wote wa Bunge la Umma la 14 la China na watu wa China wa makabila yote.

“Katika safari mpya inayokuja, China itaendeleza bila kuyumba maendeleo yenye ubora wa juu” Rais Xi amesema.

Rais Xi amesema wazo la maendeleo yanayowapa kipaumbele cha juu watu lazima litekelezwe ili mafanikio ya maendeleo ya kisasa ya China yawanufaishe watu wote kwa haki, na kwamba maendeleo makubwa zaidi yatapatikana kupitia kukuza ustawi kwa wote.

Rais Xi pia amesisitiza kuimarisha na kupanua umoja mkubwa wa watu wa makabila yote wa China na umoja mkubwa wa Wachina wote wa ndani na nje.

"Kwa kufanya hivyo, tutakusanya mambo yote yanayofaa na kuunda nguvu kubwa ambayo itawezesha ujenzi wa nchi kubwa ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa na kuendeleza ustawishaji wa Taifa la China," Rais Xi amesema.

Rais Xi pia amesisitiza kufanya juhudi za kuendeleza maendeleo ya kisasa katika ulinzi wa taifa na vikosi vya kijeshi katika nyanja zote, na kujenga majeshi ya umma ya China kuwa "Ukuta Mkuu wa chuma" ambao unaweza kulinda kikamilifu mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo ya Taifa la China.

Rais Xi pia amesisitiza kuteketelezwa kikamilifu kwa sera ya “Nchi Moja, Mifumo Miwili” huko Hong Kong na Macao na kufuata kikamilifu kanuni ya kuwepo kwa China moja na Makubaliano ya Mwaka 1992, kuhimiza kikamilifu maendeleo ya amani ya uhusiano kwenye Mlango Bahari wa Taiwan na kupinga kwa uthabiti uingiliaji wa nje na shughuli za makundi yanayotaka Taiwan ijitenge na China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha