Wadhibiti wa Marekani waifunga Benki ya Signature ya New York baada ya kuanguka kwa Benki ya Silicon Valley (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 14, 2023
Wadhibiti wa Marekani waifunga Benki ya Signature ya New York baada ya kuanguka kwa Benki ya Silicon Valley
Mlinzi akionekana ndani ya tawi la Benki ya Signature huko New York, Marekani, Machi 13, 2023. (Xinhua/Zhang Mocheng)

NEW YORK - Benki ya Signature ambayo makao yake makuu yako New York, Marekani ni benki muhimu ya sekta ya sarafu ya mtandaoni, imefungwa siku ya Jumapili na wadhibiti wa serikali ya Marekani kwa "sababu maalum za hatari sawa za kimfumo," Wizara ya Fedha ya Marekani, Benki Kuu ya Marekani, na Shirika la Bima ya Amana la Marekani (FDIC) zimesema katika taarifa ya pamoja.

Hatua hiyo imekuja siku mbili baada ya Benki ya Silicon Valley ya California (SVB) kuanguka huku wawekaji pesa wakikimbilia kutoa pesa zao.

Wawekaji pesa wote wa Benki ya Signature "watalipwa kiasi chao chote," imesema taarifa hiyo ya pamoja. "Kama ilivyo kwa azimio la Benki ya Silicon Valley, hakuna hasara itakayobebwa na walipa kodi."

Mamlaka hizo pia zimesema "wanahisa na wadaiwa fulani ambao hawajalindwa hawatalindwa."

Kwa mujibu wa taarifa tofauti iliyotolewa Jumapili jioni na Idara ya Huduma za Kifedha ya New York, Benki ya Signature ikiwa ilianzishwa Mwaka 2001, ni benki ya kibiashara iliyopata ruhusa maalum ya Serikali ya New York na imewekewa bima ya FDIC, ikiwa na jumla ya mali zenye thamani ya takriban dola za Marekani bilioni 110.36 na amana za jumla zenye thamani ya takriban dola bilioni 88.59 kufikia Desemba 31, 2022.

Serikali ya Jimbo la California iliifunga SVB siku ya Ijumaa baada ya benki hiyo iliyojikita katika sekta ya teknolojia kuripoti hasara kubwa kutokana na mauzo ya dhamana, na kusababisha wateja wengi kwenda haraka kuchukua akiba za benki hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha