Mjumbe wa China katika UN asema chuki dhidi ya China itasababisha migogoro na mapambano

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 15, 2023
Mjumbe wa China katika UN asema chuki dhidi ya China itasababisha migogoro na mapambano
Geng Shuang (kushoto, mbele), Naibu Mwakilishi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa, akizungumza katika Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Ukraine katika muktadha wa chuki dhidi ya Russia, Russophobia uliofanyika huko New York, Machi 14, 2023. Mjumbe huyo wa China ameonya Jumanne kwamba chuki dhidi ya China, Sinophobia inayooneshwa na wanasiasa itasababisha migogoro na mapambano. (Xinhua/Xie E)

UMOJA WA MATAIFA, - Naibu Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa, Geng Shuang ameonya Jumanne kwamba chuki dhidi ya China, yaani Sinophobia inayooneshwa na wanasiasa itasababisha migogoro na mapambano.

"Hivi sasa, watoa muhtasari wa Baraza la Usalama walieleza maoni yao kuhusu Russophobia (chuki dhidi ya Russia), na uhusiano wake na mgogoro wa Ukraine. Ningependa kuchukua fursa hii kueleza kwamba kwa muda sasa, wanasiasa katika baadhi ya nchi wanaonekana kuwa na hali ya Sinophobia." amesema mjumbe huyo.

Wanasiasa hao wamejaa chuki na wasiwasi kuhusu China, kunadi hofu, na kuchochea mivutano. Sinophobia kama hiyo ni matokeo ya kutoielewa vema China, uamuzi mbaya wa kimkakati, na ghiliba za kisiasa, ameuambia mkutano wa Baraza la Usalama kuhusu Ukraine katika muktadha wa chuki dhidi ya Russia, Russophobia.

Geng amesema, sera ya Nchi ya China, ikiwa itatekwa nyara na chuki dhidi ya China, Sinophobia, itasababisha tu kuzidisha mchezo wa kutiana hasara, na kuzuia na kukandamiza, na hivyo kusababisha migogoro na mapambano.

"Dunia tayari imetupwa katika machafuko kutokana na mgogoro wa Ukraine. Je, mgogoro mwingine unapaswa kuundwa ili kuifanya Dunia kuwa nje ya kutambuliwa?" ameuliza.

"Kwa maendeleo ya jamii ya watu hadi hapa yalipo, tunapaswa kukomaa vya kutosha kuweza kusikiliza sauti tofauti na kukumbatia mawazo na ustaarabu tofauti. Dunia ni kubwa kuweza kutosha kwa nchi zote kukua pamoja na kufikia maendeleo kwa pamoja," amesema.

Kuhusu mgogoro wa Ukraine, Geng ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendeleza mazungumzo ya amani.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha