China yauanza Mwaka 2023 kwa uchumi unaoimarika kwa nguvu (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 16, 2023
China yauanza Mwaka 2023 kwa uchumi unaoimarika kwa nguvu
Picha hii iliyopigwa Tarehe 2 Machi 2023 ikionyesha mitambo ya kuzalisha umeme kwa nishati ya upepo itakayosafirishwa katika Bandari ya Yantai huko Yantai, Mkoa wa Shandong nchini China. (Picha na Tang Ke/Xinhua)

BEIJING - Uchumi wa China umeanza kukua kwa kasi ya juu Mwaka 2023, huku viashiria vikuu vya uchumi vikishuhudia upanuzi wa kasi, vikitoa ushahidi wa hivi punde kwamba uchumi wa nchi hiyo yenye uchumi wa pili kwa ukubwa duniani unatazamiwa kupata hali nzuri yenye nguvu mwaka huu.

Takwimu zilizotolewa Jumatano na Idara ya Takwimu ya kitaifa ya China imeonesha kuwa, Pato la ongezeko la thamani la viwanda nchini China limepanda kwa asilimia 2.4 kutoka kiwango cha mwaka jana katika miezi miwili ya kwanza .

Ukuaji huo umepanda kwa asilimia 1.1 kutoka kiwango cha Desemba, Mwaka 2022, na wastani wa ukuaji wa miaka miwili umefikia asilimia 4.9.

Uuzaji wa bidhaa za matumizi kwa reja reja nchini China uliongezeka kwa asilimia 3.5 kuliko ule wa mwaka uliopita katika kipindi hicho, na hivyo kurudisha nyuma ukuaji wa chini ulioonekana katika miezi mitatu iliyopita. Uuzaji wa bidhaa zinazoboresha matumizi kama vile vito ulipanuka haraka. Na viashiria vingine vikuu vya kiuchumi, vikiwemo uwekezaji wa mali zisizohamishika na fahirisi ya uzalishaji wa huduma, pia vimeonyesha ukuaji kuliko mwaka jana.

"Katika miezi miwili ya kwanza, uchumi wa China umeimarika kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya uzalishaji, ajira imara na bei za walaji, na kuboresha matarajio ya soko," Msemaji wa Idara ya Takwim ya Kitaifa Fu Linghui ameuambia mkutano na waandishi wa habari.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha