Xi Jinping ahimiza vyama vya siasa kuongoza lengo la maendeleo ya kisasa, apendekeza Mpango wa Ustaarabu wa Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 16, 2023
Xi Jinping ahimiza vyama vya siasa kuongoza lengo la maendeleo ya kisasa, apendekeza Mpango wa Ustaarabu wa Dunia
Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Rais wa China, akihudhuria na kutoa hotuba kwa njia ya video kwenye Mkutano wa Mazungumzo wa ngazi ya juu kati ya Chama cha CPC na Vyama vya Siasa Duniani hapa Beijing, Mji Mkuu wa China, Machi 15, 2023. (Xinhua/Huang Jingwen)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), ametoa wito kwa vyama vya siasa duniani kuoanisha kwa karibu maendeleo yao wenyewe na mikakati yao ya kufikia mambo ya kisasa ya kitaifa, ili kuendelea kuongoza lengo na nguvu kubwa ya maendeleo ya kisasa.

Rais Xi alitoa wito huo siku ya Jumatano kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Mazungumzo kati ya CPC na Vyama vya Siasa Duniani uliofanyika kwa njia ya video.

Wajibu wa Vyama vya Siasa

Rais Xi amesema katika hotuba yake kwamba katika Dunia ya leo, changamoto na migogoro mingi vimesongamana, na mchakato wa maendeleo ya kisasa ya binadamu umefikia tena njia panda ya historia.

Vyama vya siasa, kama nguvu muhimu inayoongoza na kuendesha mchakato wa maendeleo ya kisasa, vina wajibu wa kujibu maswali kama vile "tunahitaji aina gani ya maendeleo ya kisasa na jinsi gani tunaweza kuyafanikisha," amesema.

Rais huyo wa China ametoa wito kwa vyama vya siasa kuwaweka watu kwenye kipaumbele cha juu na kuhakikisha maendeleo ya kisasa yanatilia maanani maslahi ya watu.

Njia ya China kuelekea maendeleo ya kisasa

Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC umependekeza kuendeleza Ustawishaji wa Taifa la China katika sekta zote kupitia njia ya maendeleo ya kisasa ya China.

Akizungumzia njia hiyo ya maendeleo ya kisasa ya China, Rais Xi amesema kwamba inajikita katika kuendana na hali halisi ya nchi ya China na pia inatokana na uzoefu wa nchi nyingine; inaleta manufaa kwa watu wa China na pia kuendeleza maendeleo ya pamoja ya Dunia.

Mpango wa Ustaarabu wa Dunia

Katika hotuba yake, Rais Xi amependekeza Mpango wa Ustaarabu wa Kimataifa.

Chini ya mpango huo, Rais Xi ametoa wito wa kuheshimiwa kwa ustaarabu mbalimbali, kutetea maadili ya kawaida ya binadamu, kuthamini sana urithi na uvumbuzi wa ustaarabu, na kutetea kwa pamoja mabadilishano na ushirikiano wa kimataifa kati ya watu na watu.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress (ANC), na viongozi wengine 11 wa vyama vya siasa na mashirika ya kisiasa pia walihutubia kwenye mkutano huo wa mazungumzo. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha