Botswana yazindua mradi wa kwanza wa photovoltaic na kilimo ili kutumia kikamilifu nishati inayotokana na mionzi ya jua (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2023
Botswana yazindua mradi wa kwanza wa  photovoltaic na kilimo ili kutumia kikamilifu nishati inayotokana na mionzi ya jua
Gari moja likizipita paneli za kuzalisha umeme kwa mwanga wa jua katika Chuo Kikuu cha Kilimo na Maliasili cha Botswana huko Gaborone, Botswana, Tarehe 15, Machi, 2023. (Picha na Tshekiso Tebalo/Xinhua)

Chuo Kikuu cha Kilimo na Maliasili cha Botswana (BUAN) kimezindua mradi unaochanganya kwa pamoja uzalishaji umeme kwa mionzi ya jua na kilimo, Agrivoltaic huko Gaborone, mji mkuu wa Botswana, Jumatano.

Mradi huo ambao ni wa kwanza wa aina yake katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ni wa ufungaji wa vifaa vya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati inayotokana na mionzi ya jua wenye nguvu ya megawati 1 na hutoa umeme kwa chuo kikuu hicho wakati wa mchana. Kulingana na bili za matumizi zilizopangwa, tathmini ya upembuzi yakinifu wa mradi ilitabiri kuwa gharama za umeme katika chuo kikuu hicho zingeshuka kwa zaidi ya asilimia 50 katika muda wa kati, na nishati yoyote ya ziada itaingia kwenye gridi ya taifa.

Makamu Rais wa Botswana, Slumber Tsogwane, alisema katika hafla ya uzinduzi kwamba uzinduzi wa mradi huo unakuja miaka miwili baada ya Mpango Jumuishi wa Rasilimali ya Umeme wa Botswana kuanzishwa, ambao unasisitiza sana maendeleo ya nishati mbadala.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha