Beijing yaanzisha huduma ya treni ya kwanza ya mizigo ya moja kwa moja kati ya China na Ulaya (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 17, 2023
Beijing yaanzisha huduma ya treni ya kwanza ya mizigo ya moja kwa moja kati ya China na Ulaya
Treni ya mizigo ya kati ya China na Ulaya inayoelekea Moscow, Russia ikiondoka kwenye stesheni ya reli ya Mafang katika Eneo la Pinggu la Beijing, Machi 16, 2023. (Xinhua/Ren Chao)

BEIJING - Treni ya mizigo iliyobeba makontena 55 imeondoka Beijing Alhamisi asubuhi kuelekea Moscow, Mji Mkuu wa Russia, ikionesha kuanzishwa kwa huduma ya treni ya mizigo ya kwanza ya moja kwa moja kati ya China na Ulaya kutoka Beijing, Mji Mkuu wa China .

Treni hiyo ya mizigo iliyobeba bidhaa kama vile vifaa vya ujenzi, vifaa vya umeme vya nyumbani na nguo iliondoka kutoka kituo kikuu cha usafirishaji mizigo cha Eneo la Pinggu, Kaskazini-Mashariki mwa Mji wa Beijing na itatoka katika mipaka ya China kupitia Bandari ya Manzhouli iliyoko katika Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China.

Treni hiyo inatarajiwa kufika Moscow ndani ya muda wa siku 18, ikisafiri kwa umbali wa takriban kilomita 9,000.

"Hapo awali, tulihitaji kupeleka bidhaa katika mikoa ya Henan au Hebei kabla ya kusafirishwa hadi Ulaya," amesema Chu Yixiao, Meneja Mkuu wa Shirika la Usafirishaji la Taitong International.

"Kwa kuanzishwa kwa huduma hii ya treni ya mizigo, sasa bidhaa zinaweza kutumwa moja kwa moja kutoka Beijing hadi Ulaya, kupunguza gharama za usafirishaji na kuongeza ufanisi wa usafirishaji," amesema, huku akiongeza kuwa maendeleo hayo yanatoa fursa mpya kwa biashara kustawi.

Mwaka huu ni mwaka wa 10 tangu kuanza kwa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI). , Mwenyekiti wa bodi ya shirika la Reli la China Liu Zhenfang amesema, treni za mizigo za kati ya China na Ulaya zimeunganisha miji 108 ya China na miji 208 katika nchi 25 za Ulaya, huku njia za mizigo zikishughulikia safari 65,000 za treni ya mizigo.

(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha